Na
Lucas Raphael,Urambo
Watu wawili kati ya sita
wamehukumiwa kifungo cha jumla ya miaka 60 jela baada ya kupatikana na hatia ya
unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya bastola na kupora kiasi cha
shilingi 380,000/=.
Akitoa hukumu hiyo hakimu
mkazi wa mahakama wilaya ya Urambo mkoani Tabora Baptista Kashusha
alisema anatoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya
kutenda makosa kama hiyo.
Alisema kwamba kutoakana na
kukidhiri kwa vitendo vya uhalifu katika maeneo ya mijini na vijijini adhabu
kali ndio fundisho pekee kwa watu wa aina hiyo.
Waliopatikana na hati hiyo ya
unyang’anyi wa kutumia silaha aina ya bastola na marungu na kufanyikiwa kupora
kiasi hicho cha fedha ni Mageta Jumanne (23) na Mhoja Mabula (27) wote ni
wakazi wa Igagala wilaya ya Kaliua.
Hata hivyo mahakama hiyo
iliwaachia huru watuhumiwa wanne kwa kukosa ushahidi wa kutosha kuweza kuwatia
hatiani ambao ni Amos Mabiika(20) ,Rashid Emanuel (25), Kadoke Msengele(24)
Peter Cherehani(38) .
Kabla ya kutolewa kwa
hukumu hiyo mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi mkaguzi msaidizi Felbet Pima
aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa washitakiwa hao iliwe iwe fundisho
kwa watu wengine.
Awali mwendesha mashitaka huyo
aliiambia mahakama hiyo kuwa mnamo tarehe 20 Januari 2015 majira ya saa 7 usiku
katika kijiji cha Mtakuja wilaya ya
kaliua mkoa wa tabora washitakiwa kwa pamoja kabla na baada ya kupora
waliitishia kwa bastola na marungu na kufanikiwa kupora kiasi cha shilingi
380,000/kutoka kwa Regina John.
No comments:
Post a Comment