![]() |
MKURUGENZI MTENDAJI WA TUWASA INJINIA MKAMA BWIRE AKIWASILISHA MADA YA UPATIKANAJI WA MAJI KATIKA MANISPAA YA TABORA MBELE YA MADIWANI WA MANISPAA HIYO |
Na Paul Chriatian, Tabora.
Imeelezwa kuwa maji ya bwawa la Igombe
yanayohudumia wakazi wa Manispaa ya Tabora hayotoweza kutosheleza mahitaji ya
watu wa Manispaa hiyo ifikapo mwaka 2019.
Akiwasilisha mada ya hali ya upatikanaji maji katika
Manispaa hiyo Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira
TUWASA injinia Mkama Bwire amesema upungufu huo wa maji utatokana na ongezeko
la idadi ya watu.
Amasema mamlaka hiyo kwa sasa inazalisha maji ya lita
za ujazo milioni 15 kwa siku, huku mahitaji halisi kwa wakazi wa Manispaa hiyo
ambao ni zaidi ya 250,000 ni lita za ujazo milioni 24.005 kwa siku.
Mkurugenzi huyo ameeleza kuwa lita hizo za ujazo
milioni 15 zinazozalishwa na mamlaka hiyo zinahudumia kata 19 kati ya kata 29
za Manispaa hiyo, huku lengo likiwa kuzifikia kata zote.
Injinia Bwire amesema Mamlaka hiyo itakuwa na
uwezo wa kuzalisha maji ya lita za ujazo milioni 30 kwa siku ifikapo mwezi
Machi mwaka huu na hivyo kuondoa mgawo
wa maji uliopo hivi sasa, baada ya kukamilika ujenzi wa machujio mapya na
kukarabati ya zamani.
Mkurugenzi huyo wa TUWASA amesema ili kukabiliana
na hali hiyo ya bwawa la Igombe kufikia ukomo wake kutosheleza mahitaji ya
wakazi wa Manispaa ya Tabora miradi ya maji kutoka ziwa Victoria na mto
Malagarasi ni muhimu kutekelezwa.
Injinia Bwire amebainisha kuwa mradi wa maji ya
ziwa Victoria umefikia hatua ya wizara ya husika kutangaza zabuni mwishoni mwa
mwaka jana ili apatikane mkandarasi wa kuifanya kazi hiyo ya kutoa maji katika
kijiji cha Solwa kilichpo Shinyanga vijijini.
Aidha amesema mradi huo utatekelezwa na
wakandarasi tofauti ambao watagawana kutoka Shinyanga-Nzega, Nzega-Tabora na
Nzega Igunga na kwamba utagharimu shilingi bilioni 279,390,444,272.19
Semina hiyo ya hali ya maji katika Manispaa hiyo imeandaliwa
na TUWASA ikiwalenga madiwani wa Manispaa hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa
kuendeleza huduma muhimu ya maji kwa wakazi wake.
No comments:
Post a Comment