Na Paul Christian, Tabora
Mbunge wa Jimbo la Ulyankulu John Peter Kadutu
ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Kaliua mkoani Tabora kumzawadia dereva wa
gari la wagonjwa (ambulance) la kituo cha afya cha Ulyankulu kufuatia kujitolea
kwa fedha zake za mfukoni kutengeneza kitanda cha kubebea wagonjwa kwenye gari
hilo ambacho hakikuwepo.
![]() |
KITANDA KILICHOTENGENEZWA KWA FEDHA ZA DEREVA ADREY |
Amesema mtumishi huyo Adrey ameonesha moyo wa
kizalendo na ari ya kipekee inayofaa kuigwa na watumishi wengine katika jimbo
hilo na kwamba anastahili kuenziwa rasmi kwa kitendo hicho.
Agizo hilo limetolewa mbele ya mwenyekiti wa
halmashauri hiyo Haruna Kasele,mwenyekiti wa kamati ya elimu, afya na maji ambaye
pia ni diwani wa kata ya Uyowa Alphonce Msanzya na mwakilishi wa Mkurugenzi
Mtendaji wa halmashauri hiyo afisa utamaduni na michezo Marko
Kapela.
No comments:
Post a Comment