Na Paul Christian,
Tabora.
Timu ya taifa ya Nigeria imeondolewa
kwenye mashindano ya ubingwa wa mataifa ya Afrika kwa timu za taifa zinazoundwa
na wachezaji wanaocheza ligi za nchi husika CHAN 2016 baada ya kukubali kichapo
cha bao 1 kwa bila kutoka kwa Guinea.
Nigeria “Super Eagle” imeondolewa
kwa kufikisha pointi 4 nyuma ya vinara wa kundi C Tunisia na Guinea
iliyojikusanyia pointi 5 baada ya ushindi wa mechi hiyo ya mwisho ya kundi
hilo.
Mchezaji wa Guinea Ibrahima Sankhon
ndiye aliyeifungia timu yake ya Guinea bao la pekee kunako dakika ya 45 ya
mchezo na kuifungashia virago Super Eagle katika mechi iliyopigwa Jumanne.
Kabla ya mechi za mwisho za kundi
hilo Super Eagle inayonolewa na Sunday Oliseh ilikuwa ikiongoza kundi hilo
ikiwa na pointi 4.
Mechi nyingine ya kundi hilo
ilizikutanisha Tunisia na Niger ambapo Tunisia imeibamiza Niger kwa magoli 5
kwa bila na kuongoza kundi hilo.
Katika kundi hilo Tunisia na Guinea
zimevuzu hatua ya robo fainali katika michuano hiyo.
Hata hivyo kocha wa Nigeria Sunday
Oliseh amewaomba radhi mashabiki wa Super Eagle na wanageria kwa kutolewa
mapema katika michuano hiyo ya CHAN 2016.
Guinea iliwakilishwa na: 16. Keita (C), 2. Thiam, 5. Bangoura, 6. Sankhon, 8. Soumah, 12. Sylla, 13. A. Camara, 15. Camara A, 17. D. Camara, 19. Youlla, 23. A.L. Camara.
No comments:
Post a Comment