Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Thursday, January 28, 2016

KAYA 2,664 ZAATHIRIKA NA MVUA UYUI



Na Hastin Liumba,Uyui

JUMLA ya nyumba 415 zimebomoka na kusombwa na maji kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha wilayani Uyui mkoani Tabora.

Mkuu wa wilaya hiyo  Zuhura Ali amesema hayo wakati akitoa taarifa ya serikali kwenye kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo kilichofanyika Isikizya wilayani humo.

Amesema licha ya kaya hizo kuathirika, jumla ya ekari 225
za mazao mbali mbali zimeaharibiwa vibaya na  mvua zinaendelea kunyesha wilayani humo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema  ekari 342 za tumbaku nazo zimaharibiwa vibaya na mvua hizo.

Amebainisha kuwa mvua hizo pia zimeathiri miundombinu ya barabara au kuyafanya maeneo kutofikika  kufuatia  barabara kufunikwa na maji.
Kuhusu kaya hizo zilizoathiriwa amesema serikali wilayani humo imechukua hatua kuhakikisha wakazi wa kaya hizo wanahifadhiwa sehemu zenye uhakika ili waweze kupata huduma muhimu za kijamii.

Zuhura amesema tayari serikali ngazi ya wilaya imetoa taarifa serikali kuu ili  ipatiwe  msaada wa dharura kwa  ajili ya wahanga hao.

Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya amebainisha kuwa ameendelea kutoa elimu kwa wananchi wa wilaya yake kuanza kujenga nyumba imara na wale wengine ambao wamejenga sehemu za mabondeni kuchukua tahadhari ikiwemo kuhama mara moja.

Amesema serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali kwa kufanya ukarabati wa muda  maeneo yasiyofikika ili yaweze kupitika kwa kutengeza barabara na madaraja.


No comments: