Na Paul Christian,Tabora
Mamlaka ya maji safi
na usafi wa Mazingira Manispaa ya Tabora TUWASA imesema wananchi wanaoshidwa
kulipa bili zao za maji kwa wakati na kusababisha kukatiwa huduma wanajikosesha
haki ya msingi ya kuishi.
Mkurugenzi mtendaji wa
mamlaka hiyo Mkama Bwire amesema baadhi ya wateja wa mamlaka hiyo kutolipia bili
zao za maji kwa wakati walipaswa
kushitakiwa kwa kosa la kutaka kujitoa uhai kwa kuwa maji ni uhai.
Mkurugenzi huyo amesema
kwa utaratibu wa sasa wateja wa mamlaka hiyo wanaposhindwa kulipia bili zao
wanasitishiwa huduma ya maji hali inayopaswa kuangaliwa upya ili iwepo sheria
ya kuwashitaki kwa makosa ya kutaka kujitoa uhai kwa kukosa huduma hiyo.
Aidha amewataka wakazi
wa Manispaa ya Tabora kuthamini umuhimu wa maji kwa kulipia bili zao, kutunza
miundombinu ya maji pamoja na kuhifadhi mazingira.
Awali akizungumza
mbele ya madiwani wa halmashauri ya manispaa hiyo mkuu wa wilaya ya Tabora Suleiman Kumchaya
amesema wadadisi wa mambo wamebashiri kuwa vita kuu ya tatu ya dunia itasababishwa
na uhaba wa maji wakati mahitaji ya binadamu na mifugo yakiongezeka kwa kasi.
No comments:
Post a Comment