NA,
Thomas Murugwa, Tabora.
Mahakama
ya wilaya ya Tabora imemtia hatiani aliyekuwa Afisa upelelezi wa wilaya ya
Sikonge Maroba Nyamsongoro na kumtaka ajibu mashitaka mawili ya kuomba na
kupokea rushwa yanayomkabili.
Hakimu
mkazi mfaidhi wa mahakama ya wilaya ya Tabora Ngigwana alitoa uamuzi huo
Alhamis baada ya kusikiliza maelezo ya ushahidi ya upande wa mashitaka uliokuwa
ukiongozwa na wakili Edson Mapalala wa Taasisisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
nchini TAKUKURU.
Ngigwan
alisema kuwa upande wa mashitaka umeweza kuthibitisha makosa ya mshitakiwa huyo
hivyo anapaswa kutoa utetezi ambao unaweza kumuokoa asipewa adhabu.
Awali
wakili Mapalala aliiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitenda makosa hayo
mawili tarehe 12 Machi,2013 wakati akiwa ni afisa upelelezi wa wilaya ya
Sikonge.
Mapalala
alisema kuwa siku hiyo mshitakiwa akiwa ni mtumishi wa serikali aliomba Tshs.
2,000,000/= toka kwa Yusuph Hemed ili asimchukulie hatua za kisheria kwa
tuhuma za kujihusisha na vitendo vya ugaidi.
Katika
shitaka la pili ilidaiwa kwa afisa upepelezi huyo wa polisi alipokea kiasi cha
Tsh. 700,000/= toka kwa malipo ya awali ili asimchukulie hatua za kisheria.
Mshitakiwa
katika kesi hiyo anawakilishwa na wakili wa kujitegemea Mugaya Mtaki.
No comments:
Post a Comment