Na Ezra Kigata,Ulyankulu.
Wakazi wa vijiji vya kata ya Ng’wande tarafa ya
Ulyankulu wilaya ya Kaliua mkoani Tabora wanatumia mitumbwi kuvuka kwenda
ng’ambo ya pili kufuata huduma muhimu za kijamii kufuatia mto Igombe kujaa maji katika kipindi
hiki cha mvua.
Wakazi hao wanavushwa kwa mitumbwi kwa gharama ya
shilingi 2,000/- kwa mtu mmoja, kuvusha pikipiki wanalipa shilingi 4,000/- hali
ambayo inawaathiri kiuchumi.
Simon Michael ni mmoja wa watu wanaofanya kazi ya
kuwavusha watu, vyombo vya usafiri na mizigo katika mto huo amesema kazi hiyo inamuingizia
kipato kinachomsaidia kukidhi mahitaji ya familia.
Hali hiyo inawaathiri zaidi wanawake, watoto,
wagonjwa na wafanyabiashara na wakazi wa kata hiyo wameitaka serikali
kuwajengea daraja kwa kuwa kimekuwa kilio chao cha muda mrefu.
No comments:
Post a Comment