Timu ya taifa ya Mali imefuzu
kucheza nusu fainali ya michuano ya CHAN 2016 kufuatia kupata ushindi wa goli 2
kwa 1 dhidi ya Tunisia katika mechi ya robo fainali iliyochezwa Jumapili.
Alikuwa Mohamed Ali Moncer
aliyeipatia Tunisia goli la kuongoza kunako dakika ya 14 ya kipindi cha kwanza
baada ya kuunganisha krosi iliyochongwa na Saad Bguir.
Katika kipindi cha pili penati
iliyopigwa na Aliou Dieng kufuatia Zied Boughattas kufanyiwa madhambi ilizaa goli la kusawazisha kwa timu ya Mali.
Kunako dakika ya 80 ya mchezo Diarra
akitokea wing ya kushoto aliingia kwenye penati box na kupiga mpira uliompita
golikipa wa Tunisia Jerid na kutumbukia nyavuni na kuandika goli la pili kwa
Mali.
Hadi mwamuzi wa kati anamaliza
pambano hilo Mali waliibuka na magoli 2 kwa 1 dhidi ya Tunisia.
Siku ya Alhamisi Mali itashuka
dimbani kuvaana na majirani zao Ivory Coast katika mechi ya nusu fainali.
Fainali itachezwa siku ya Jumapili
ijayo.
![]() |
GUINEA WAKISHANGILIA |
Mechi
hiyo iliyochezwa kwenye uwanja wa Umuganda, Rubavu, timu zote zilimaliza dakika
90 za kawaida bila kufungana na mwamuzi wa kati raia wa Ethiopia Bamlak Tessema
aliongeza dakika 30 ambapo zilimaliza bila kufungana kwa mara nyingine.
Mikwaju
ya penati iliamuliwa ili apatikane
mshindi, Guinea walifunga penati zao kupitia kwa Ibrahima Bangoura, Mohamed
Thiam, Issiaga Kamara, Ibrahima Soumah na goalkeeper Abdol Azizi Keita ambapo
Douda Kamara na Ibrahim Sankhin walipoteza penati zao.
Kwa upande wa Zambia, Buchizya Mfuma, Spencer
Sautu,Cleotus Chama na Adrian Chama waliwafanyikiwa kukwamisha nyavuni penati
zao, huku Christopther Katongo, Stephene Kabamba na Daut Musekwa wakikosa
penati zao.
Kwa ushindi huo Guinea itakutana na Congo DR
katika mechi ya nusu fainali itakayochezwa siku ya Alhamisi wiki hii.
No comments:
Post a Comment