![]() |
IGP ERNEST MANGU |
Na Paul Christian,Kaliua
Askari polisi wa
wilaya ya Kaliua mkoani Tabora wameaswa kuacha tabia ya kuvujisha taarifa za
siri kuhusu wahalifu wanazopewa na raia wema ili kukabiliana na matukio ya
uhalifu wilayani humo.
Rai hiyo imetolewa
hivi karibuni na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua Haruna Kasele
alipokuwa akizungumza na askari polisi wa tarafa ya Ulyankulu wilayani humo.
Amesema baadhi ya
askari hao wamekuwa na tabia ya kuvujisha kwa watuhumiwa taarifa za siri
wanazopewa na wananchi jambo ambalo limehatarisha maisha na mali za raia hao
kwa kulipiziwa visasi.
Kasele amesema vitendo
hivyo ambavyo ni kinyume na maadili ya jeshi la polisi vimekuwa vikiwasaidi
wahalifu kuharibu au kuficha ushahidi na
hivyo raia wema kuonekana waongo.
Mwenyekiti huyo wa
halmashauri amesisitiza kuwa endapo askari polisi wilayani humo watafanya kazi
kwa misingi ya maadili wananchi wako tayari kutoa ushirikiano wa kuwafichua
wahalifu.
No comments:
Post a Comment