![]() |
EDGAR NA DENNIS (ALIYEVAA HEADPHONE) WATANGAZAJI WA MEZA HURU VOT FM STEREO |
![]() |
RTO MICHAEL DELELI |
Na Paul Christian, Tabora.
Jeshi la polisi mkoani Tabora limemewataka
madereva wa vyombo vya moto kuepuka kufanya makosa ya kibinadamu ili kuepusha
ajali barabarani.
Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Tabora (RTO), SP Michael Deleli
ameyasema hayo leo asubuhi alipokuwa akihojiwa kwenye kipindi cha Meza Huru
kinachorushwa na VOT FM STEREO.
Amesema madereva wote wanapaswa kuepuka vitendo
vya kunywa pombe kulewa na kuendesha vyombo vya moto,kutokuwa na mafunzo ya
udereva, kuongea kwa simu wakati wanaendesha,
kuendesha magari mabovu, kutoheshimu alama za barabarani, kutoheshimu sheria za
usalama barabarani pamoja na matumizi sahihi ya taa za vyombo hivyo.
Deleli amebainisha kuwa makosa ya kibinadamu
yanayofanywa na madereva wanapokuwa wanaendesha vyombo vya moto yamechangia
kutokea kwa ajali ambazo zimesababisha vifo na majeruhi wengi.
Mkuu huyo wa kitengo cha usalama barabarani mkoa
wa Tabora amesema katika kukabiliana na hali hiyo mwaka 2015 zaidi ya madereva
900 walipatiwa mafunzo ya udereva kwa kushirikiana na vyuo vya mafunzo ya
udereva pamoja na mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA.
Aidha amewaonya wamiliki wa magari yanayotoa
huduma za usafirishaji mkoani Tabora kuacha tabia ya kubadili muundo wa viti
vya magari yao kwa lengo la kubeba abiria wengi pamoja na mizigo.
Deleli amebainisha hatua hiyo ya wamiliki wa
magari hayo ni uvunjaji wa sheria za nchi na kwamba hatua za kisheria
zitachukuliwa kwa wale watakaobainika.
No comments:
Post a Comment