Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, January 17, 2016

MIAKA 55 YA KUMBUKUMBU YA PATRICE LUMUMBA



 
PATRICE LUMUMBA 1925-1961
Na Paul Christian, Tabora.

Jumapili ya tarehe 17 mwezi huu ilikuwa  siku ya kumbukumbu miaka 55 ya kifo cha waziri mkuu wa kwanza wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo Patrice Lumumba.

Patrice Lumumba alizaliwa Julai 2, 1925 Katakokombe na kuuawa kikatili na kwa maumivu makali Elisabethville kwa sasa (Lubumbashi) tarehe 17 January,1961 akiwa na umri wa miaka 35 tu.

Kiongozi huyo wa kwanza wa taifa hilo aliongoza chama cha Congolese National Movement MNC.

Kifo chake kiliratibiwa na kutekelezwa na wakoloni wa taifa hilo Ubelgiji wakishirikiana na Marekani kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kujihusisha moja kwa moja na suala la kuomba msaada kutoka Urusi.

Patrice Lumumba na chama chake kilishinda uchaguzi uliofanyika  kuanzia tarehe 11 hadi 25 Mei 1960 na hivyo Congo DRC kupata uhuru wake tarehe 30 Juni, 1960.

Kiongozi huyo atakumbukwa kwa msimamo wake, kutokuwa na woga, kupinga ubeberu na kuwa na wazo la kuiona Afrika huru na siku moja kuwa Taifa moja “The State of Africa”.

No comments: