Na Paul Christian, Tabora
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh. Job Ndugai ametangaza majina ya wabunge katika kamati za kudumu za Bunge la 11 kwa lengo la kutekeleza vyema
madaraka yake.
Kwa upande wa wabunge wa mkoa wa Tabora, mbunge wa
jimbo la Nzega mjini Mhe. Hussein Mohamed Bashe na mbunge wa jimbo la Urambo
Mashariki Mh. Margaret Simwanza Sitta wamepangwa kuwa wajumbe wa kamati ya
Huduma na Maendeleo ya Jamii.
Mbunge wa Jimbo la Tabora mjini Mhe. Emmanuel
Adamson Mwakasaka ni mjumbe wa kamati ya katiba na sheria na mbunge wa viti
maalum mkoa wa Tabora Mhe. Munde Abdallah Tambwe amekuwa mjumbe wa kamati ya Hesabu
za Serikali (PAC).
Mbunge wa Jimbo la Sikonge Mhe. Joseph George
Kakunda pamoja na mbunge wa jimbo la Bukene Mhe. Selemani Jumanne Zeddy wameteuliwa
kuwa wajumbe wa kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma ambapo mbunge wa jimbo la
Igalula Mhe. Mussa Rashid Ntimizi amepangiwa kamati ya Miundombinu.
Wengine ni mbunge wa jimbo la Ulyankulu John Peter Kadutu ameteuliwa kuwa
mjumbe wa kamati ya Masuala ya UKIMWI na mbunge wa jimbo la Manonga Mhe. Seif
Khamis Said Gulamali amepangiwa kuwa mjumbe wa kamati ya Hesabu za Serikali za
Mitaa (LAAC).
Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Mhe. Almas
Athuman Maige ameteuliwa kuwa mjumbe wa kamati ya Sheria Ndogo ambaye pia ni
mjumbe wa kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge ambapo Mbunge wa jimbo
la Igunga Mhe. Dkt Dalali Peter Kafumu amekuwa
mjumbe wa kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora Mwanne Ismail
Mchemba amepangiwa kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa na mbunge wa jimbo la
Kaliua Mhe. Magdalena Hamis Sakaya amekuwa mjumbe wa kamati ya Ardhi, Maliasili
na Utalii ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya Kanuni za Bunge.
No comments:
Post a Comment