Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, January 17, 2016

BARAKA DA PRINCE AFANYA VIDEO NCHINI KENYA KUONGEZA LADHA



Na Deogratius Yagomba, Tabora.

Msanii wa muziki wa kizazi kipya maarufu kama “bongo fleva” Baraka da Prince amesema anaamini ataendelea kuzikonga nyoyo za mashabiki wa muziki huo kwa mwaka 2016.

Kauli hiyo ya kujiamini ameitoa Jumamosi  wakati akifanya mahojiano ya moja kwa moja kwa njia ya simu katika kipindi cha Weekend Blast kinachorushwa na VOT FM STEREO kuanzia majira ya saa 4:15 hadi saa 7:00 usiku kila Jumamosi.

Msanii huyo anayetamba na vibao mbalimbali amesema katika kukoleza ladha ya muziki wake ameamua kutengeneza video mpya na mtayarishaji kutoka nchini Kenya Kelvin Bosco na ameiachia terehe 16 mwezi huu.

Baraka da Prince ametamba na vibao mbalimbali ikiwemo Jichunge, So fine,Siachani nawe na Nivumilie ambacho amemshirikisha msanii wa kike Ruby.

Weekend Blast ya VOT FM STEREO inamtakia kila la heri msanii huyo katika kufikia kilele cha mafanikio.

No comments: