![]() |
Rais wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli |
Na Hastin
Liumba,Kaliua
CHAMA cha wananchi (CUF) wilaya ya
Kaliua mkoani Tabora kimempongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza sera za upinzani.
Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Kaliua
Lubaga Katwiga alisema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari wilayani
humo.
Katwiga alisema hatua anazochukua
Rais Magufuli kwa sasa zilikuwa ni sehemu ya sera na ilani ya vyama vilivyokuwa
vinaunda umoja wa katiba ya wananchi UKAWA.
Alisema endapo UKAWA
ungeshinda uchaguzi wa Oktoba 25,2015 hayo anayoyafanya Magufuli yangetekelezwa
na wao ikiwa ni sehemu ya kushughulikia kero za wananchi.
Aidha mwenyekiti huyo alichukua
nafasi hiyo kuwapongeza wananchi wa jimbo la Kaliua kwa kumchagua mbunge toka
chama cha wananchi CUF Magdalena Sakaya.
Katwiga alisema mbunge huyo ni
chaguo sahihi kwa wanakaliua kwani ni mtu makini na mfuatiliaji wa kero za
wananchi na kuzipatia ufumbuzi.
Mwenyekiti huyo wa CUF alisisitiza
kuwa wananchi wa jimbo hilo watarajie mabadiliko ya kiuchumi, kisiasa na
kijamii chini ya uongozi wa mbunge huyo na kwamba hawatajuta kumchagua.
No comments:
Post a Comment