Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Tuesday, January 26, 2016

SAKAYA ACHANGIA SHILINGI MILIONI MOJA UJENZI WA SHULE KALIUA


 
MBUNGE WA KALIUA MAGDALENA SAKAYA
Na Hastin Liumba,Kaliua

MBUNGE wa jimbo la Kaliua mkoani Tabora Magdalena Sakaya amechangia
kiasi cha shilingi 1,000,000/= kusaidia  ujenzi wa shule ya msingi Miti Mitano iliyoko kata ya Usenye wilayani humo.

Sakaya amechangia kiasi hicho cha fedha ikiwa ni utekelezaji wa ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni kwa ajili ya kata hiyo


Amesema ametoa fedha hizo ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kukabiliana na kero mbalimbali zinazoikabili sekta ya afya,kilimo, wafugaji, elimu na ukosefu wa ajira kwa vijana ikiwemo bodaboda kupatiwa leseni za biashara.

Mbunge huyo wa Kaliua amesema atatumia fedha za mfuko wa jimbo kutatua kero mbalimbali inazozikabili  sekta hizo ili kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma katika jimbo hilo.

Diwani wa kata ya Usenye Madebo Hamis Juma amesema mchango huo umekuja wakati muafaka kwani kata yake ni mpya na haikuwa na shule ya msingi wala sekondari.

Amesema kata yake ina watoto 349 ambao wanatumia vyumba viwili
vya madarasa vilijengwa kwa nguvu za wananchi.

Madebo  amemshukuru mbunge huyo kwa mchango huo ambao utasukuma
ujenzi wa shule hiyo kabla ya kuanza ujenzi wa sekondari  ya kata hiyo kwani watoto wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilometa saba kuifuata shule ya sekondari iliyoko kata ya Usinge.

Vyumba hivyo hadi sasa vimegharimu kiasi cha shilingi 558,000/- kutoka shilingi 992,000/- zilizochangwa na wananchi ambapo kila mkazi amechangia shilingi 4,000/-.

Amesema kata hiyo ina jumla ya wakazi 976 na kati ya hao 248 wamechangia na 728 bado hawajachangia kutokana na sababu mbalimbali.

Amesema ujenzi wa shule hiyo ulianza  Disemba 25, 2015 na wamekusudia kuukamilisha ifikapo mwezi juni mwaka huu ili watoto wote watumie vyumba vilivyokamilika.





Top of Form
Bottom of Form


No comments: