![]() |
Wakazi wa Tarafa ya Ulyankulu wakiwa kwenye kituo cha afya Ulyankulu |
Kituo cha afya cha Ulyankulu kimeelezwa kuwa cha
mfano wilayani Kaliua kwa kutolalamikiwa na wananchi kuhusu huduma zake.
Kauli hiyo ilitolewa na mbunge wa jimbo jipya la
Ulyankulu wilayani humo John Peter Kadutu akiungwa mkono na mwenyekiti wa
kamati ya elimu, afya na maji ya halmashauri ya wilaya ya Kaliua ambaye pia ni
diwani wa kata ya Uyowa katika tarafa ya Ulyankulu Alphonce Msanzya.
Mbunge huyo amesema hajawahi kupokea malalamiko
juu ya huduma zinazotolewa katika kituo hicho cha afya licha ya kukabiliwa na
changamoto mbalimbali.
“Tangu nikiwa diwani wa kata ya Ichemba na baadaye
mwenyekiti wa kwanza wa halmashauri ya wilaya ya Kaliua, sijawahi kupokea
malalamiko ya aina yoyote kutoka kwa wananchi kuhusu huduma zenu.” Amesema kiongozi
huyo.
Kadutu amebainisha kuwa zahanati iliyoko katika kijiji anachoishi cha
Ichemba imekuwa ikilalamikiwa kwa huduma zake tofauti kabisa na kituo hicho cha
afya ambacho kinahudumia watu wengi.
Aidha ameupongeza uongozi wa kituo hicho cha afya
kwa kuzingatia usafi kwa kuyafanya mazingira kuwa nadhifu wakati wote bila
kujali wakati wa ujio wa wageni.
![]() |
Kaimu Mganga Mfawidhi Lazaro Jeremia (aliyeinua mikono) akifafanua Jambo |
Kaimu mganga mfawidhi wa kituo hicho cha afya Lazaro
Jeremia amesema kituo hicho kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo ukosefu
wa maji ya uhakika,umeme,upungufu wa dawa, vifaa tiba, watumishi,kutokuwa na
huduma ya kuongeza damu,ubovu wa barabara inayoelekea katika kituo hicho pamoja
na stahili za watumishi.
No comments:
Post a Comment