![]() |
AFISA WA SUMATRA MKOANI TABORA JOSEPH ZOMBWE MICHAEL |
Na Paul Christian, Tabora.
Mamlaka
ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini SUMATRA mkoani Tabora imetangaza
utaratibu mpya wa kutoa leseni kwa wafanyabiashara wa usafirishaji.
Akizungumza
na VOT FM STEREO leo asubuhi afisa wa SUMATRA mkoa wa Tabora Joseph Zombwe
amesema utaratibu wa sasa unaotumika ni wa kimtandao ambao unahitaji
mfanyabiashara kukamilisha taratibu zote muhimu kabla ya kupewa leseni yake.
Amezitaja
taratibu hizo kuwa ni pamoja na kulipa kodi za TRA, hati ya malipo ya Bima,
hati ya ukaguzi wa polisi,kadi ya gari, leseni ya dereva pamoja na mkataba
baina ya mfanyabiashara na dereva husika.
Zombwe
amesema utaratibu huo mpya unalengo la kuiongezea serikali mapato, kukwepa kughushi
leseni pamoja na kuhakikisha wadau muhimu wanatimiza majukumu yao ipasavyo.
Afisa
huyo wa SUMATRA mkoani Tabora amewataka wafanyabiashara wa usafirishaji
kutimiza vigezo hivyo mapema kabla ya kufika kuomba leseni au kuongeza muda wa leseni.
Zombwe
amebainisha kuwa utaratibu huo mpya unamruhusu mfanyabiashara kuanza mchakato
wa kuomba leseni yake kuongezewa muda mwezi mmoja kabla ya kufikia tarehe ya
mwisho.
No comments:
Post a Comment