Na,Thomas
Katobhaya, Tabora
Watu sita wakiwemo watendaji wa vijiji na walimu
wamehukumiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya shilingi
laki tano baada ya kupatikana na hatia ya Rushwa katika kesi mbili
tofauti.
Adhabu hiyo
imetolewa na hakimu mkazi wa mahakama ya mkoa wa Tabora Jackton Rushwela baada
ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka ulioongozwa na wakili Edson Mapalala wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU.
Waliopewa
adhabu hiyo ni Linso Mohamed ( mtendaji kata ya Ibiri),Sad Mdewa (mtendaji
kijiji cha Mkalya), Mapalala Shaban (mtendaji kijiji cha Ibiri) Adam Nassoro
(mgambo), Saada Juma Mrisho na Salma Ally Ngozi wote walimu.
Awali
Katika kesi ya kwanza iliyokuwa inawakabili maafisa watendaji ilidaiwa na
upande wa mashitaka kuwa walitenda makosa ya kushawishi na kupokea rushwa tarehe
4 Aprili 2012 katika kata ya ibiri wilaya ya Uyui.
Wakili
wa TAKUKURU alidai kuwa siku hiyo mshitakiwa Mapalala Shabani
aliomba rushwa ya shilingi milioni nne toka kwa Rukuba Masalu ili asimchukulie
hatua za kisheria kwa kosa la mifugo yake kuharibu mazao.
Katika
shitaka la pili lililokuwa linawakabiri washitakiwa wote wanne ilidaiwa na
wakili Edson kuwa walipokea rushwa ya Tsh. milioni 3.2 toka kwa Rukuba.
Hadi
mahakama inamaliza shughuli zake ni mshitakiwa mmoja tu kati yao Said
Mdewa ambaye alikuwa ameishalipa faini ya shilingi laki tano na kuwaacha
wenzake wakipelekwa gerezani hadi hapo ndugu zao watakapolipa kiasi hicho cha
fedha.
Nao
walimu wawili wa shule ya msingi Mabatini ya mjini Tabora waliotiwa hatiani kwa
makosa mawili ya kumdanyanya mwajiri pamoja na kughushi walifanikiwa kulipa
faini hivyo kukwepa adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela.
Awali
ilidaiwa na wakili Edson kuwa walitenda makosa hayo ya kumdanganya
mwajiri na kisha kughushi nyaraka wakati wakiwa ni watumishi wa serikali katika
idara ya Elimu mwezi Novemba 2008.
Ilidaiwa
kuwa siku hiyo wakiwa ni watumishi walighushi majina kwamba watu 30
wamehudhuria mafunzo ya siku tano wakati wakijua kuwa huo ni uongo
kwani mafunzo hayo yalifanyika kwa siku moja.
No comments:
Post a Comment