Timu
ya Taifa ya Congo DR imekuwa ya kwanza kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano
ya CHAN 2016 inayoendelea nchini Rwanda baada ya kuwaondosha wenyeji Rwanda kwa
ushindi wa goli 2 kwa 1 katika mechi ya kwanza ya robo fainali ya Michuano hiyo
iliyocheza Jumamosi.
Iliwachukua
dakika 11 tu kwa Congo DR kupata bao la kuongoza kupitia kwa Doxa Gikanji
aliyeachia shuti kali la mbali na kujaa nyavuni mwa Rwanda.
Licha
ya Congo DR kucheza kwa nguvu na kushambulia mara kwa mara lango la wapinzani
wao, Rwanda waliweza kuzuia na kulazimisha kipindi cha kwanza kumalizika wakiwa
nyuma kwa goli moja.
Kipindi
cha pili mashabiki wa Rwanda walilipuka kwa shangwe kufuatia mchezaji
Jean-Claude Iranzi kuisawazishia timu yake ya Rwanda na kuifanya kumaliza
dakika 90 kwa sare ya 1 kwa 1.
Chui
hao wa Congo DR walicheza na kuumiliki mchezo katika kipindi cha pili cha muda
wa nyongeza wa dakika 30 na kufanyikiwa kupata goli la pili kupitia kwa Padou
Bompunga baada ya walinzi wa Rwanda kufanya makosa.
Mechi
ya pili ya robo fainali iliwafanya Ivory Coast kuhitaji muda wa nyongeza baada
ya muda wa kawaida wa dakika 90 kumalizika bila kufungana na Cameroon.
Muda
huo wa nyongeza wa dakika 30 waliutumia vizuri na kuweza kufunga magoli 3 ya
haraka, na hivyo kufuzu hatua ya nusu fainali kwa kuibwaga Cameroon kwa magoli
3 kwa 0.
Mechi
zingine za robo fainali zitachezwa leo Jumapili kwa kuzikutanisha
- Tunisia vs Mali – katika uwanja wa Nyamirambo,Kigali
- Zambia vs Guinea – kwenye uwanja wa Umuganda ,Rubavu
No comments:
Post a Comment