Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Tuesday, January 19, 2016

MANOTA DE HUNTER KUFANYA UZINDUZI WA NYIMBO YAKE "MKWANJA"



 
DJ MAN FIMBO
Na Paul Christian, Tabora

Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa mjini Tabora Manota De Hunter atafanya uzinduzi wa Video yake Mpya inayokwenda kwa jina la “Mkwanja” kwenye Ukumbi wa buradani wa 101 wa Mjini hapa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Extra Ordinary kilichorushwa Jumanne na VOT FM STEREO Mwenyekiti wa Tanzanite Entertainment ambaye pia ni Afisa habari wa Umoja wa Vikundi vya Sanaa Tabora UVISATA Antony Mrope “Mrope Junior” amesema uzinduzi huo utafanyika tarehe 23 Jan 2016 kuanzia majira ya saa 2 usiku kwenye ukumbi huo wa 101.

Amesema UVISATA umeamua kumuunga mkono msanii huyo ili kuonyesha njia kwa wasanii wengine wa fani mbalimbali kuwa umoja huo unalengo la kuwaleta pamoja wasanii wote ili waweze kujitambua na kuendeleza vipaji vyao katika sanaa.

Mtunza hazina wa UVISATA Mohamed Ally amesema uzinduzi huo umepewa jina la “Usiku wa Mkwanja” na kwamba kiingilio kitakuwa Shilingi 5,000/=
 
MTANGAZAJI WA EXTRA ORDINARY MC ZUBBE
Mohamed ameongeza kuwa usiku huo wa "Mkwanja" utapambwa na wasanii wengine akiwemo Sultan King, Nassir Wavanilla kutoka jijini Dar es Salaam pamoja na wasanii wa fani mbalimbali kutoka mkoani Tabora.
 

No comments: