Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Friday, January 8, 2016

JE HII NI AJALI AU………….. 4 JOHNS



 
Kutoka kulia JOHN Malela,JOHN Kadutu na Jafael Lufungija
 
Na Paul Christian, Kaliua

Nimetembelea kata ya Kanoge iliyopo  Tarafa ya Ulyankulu wilaya ya Kaliua mkoani Tabora nakutana na mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa kata hiyo JOHN Simon Malela.

Mwenyekiti huyo kwa ujasiri anasema, “wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25 mwaka jana mimi nilikuwa mkurugenzi wa kampeni katika kata yangu.”

Anasema katika kipindi hicho cha kampeni alimnadi mgombea udiwani kata ya Kanoge kwa tiketi ya CCM JOHN Vicent Kahanga, wakati huo huo akimuombea kura mgombea ubunge katika jimbo la Ulyankulu kwa tiketi ya CCM JOHN Peter Kadutu pia aliwaomba wapiga kura kumchagua mgombea Urais kwa tiketi ya CCM JOHN Pombe Magufuli.

Mwenyekiti huyo anajivunia tukio la yeye pamoja na wagombea wa nafasi hizo wakitumia jina moja la JOHN na kwamba wagombea walishinda katika nafasi zao. CCM OYEEEE!!!!!!!!!

No comments: