Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Saturday, December 26, 2015

WAKAZI WA TABORA WATAKIWA KUCHANGIA DAMU




 Afisa tawala na utumishi wa Mpango wa Taifa wa Damu Salama kanda ya Magharibi NBTS Bwana Ludovick Mlay amekiri kuwepo kwa upungufu wa Damu Salama katika hospitali na vituo vya afya katika maeneo yanayohudumiwa na Mpango huo wenye makao yake mjini Tabora.

Ameitaka jamii kujenga utamaduni wa kuchangia Damu mara kwa mara ili kuokoa maisha ya watu wanaohitaji huduma ya kuongezewa Damu Salama wakati wa matibabu na ameyataja makundi yanayohitaji Damu kwa wingi ni akinamama wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Amebainisha kuwa Benki ya Damu inalojukumu la kuhakikisha Damu anayoongezewa mgonjwa imepimwa na haina vimelea vya homa ya Ini B na C, Kaswende au Virusi vya UKIMWI


Sehemu ya vifaa vya kisasa vya Maabara ya Benki Damu iliyopo mjini Tabora. Vifaa hivyo vinauwezo wa kubaini Virusi vya Ukimwi katika Damu ndani ya siku 14.
Damu ambayo iko tayari kwa kupelekwa Maabara kwa ajili ya vipimo
                                                                                                                                                                                 
Meneja wa Maabara ya Kitete Abdallah Haruna
Meneja wa maabara ya hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete Abdallah Haruna amesema hospitali hiyo kwa sasa inapokea wastani wa Unit 5 za Damu Salama kwa siku wakati kutoka Benki ya Damu Salama wakati mahitaji halisi ni wastani wa Unit 15 hadi 20 kwa siku.

Ameitaka jamii kuchangia Damu kwenye Mpango wa Taifa wa Damu Salama kwa lengo la kuokoa maisha ya wagonjwa wanaohudumiwa na hospitali hiyo ya Rufaa.

Amesema katika kukabiliana na upungufu huo wa Damu, ndugu wa wagonjwa wanalazimika kujitolea Damu baada ya kujaza fomu maalum.


No comments: