Na Catherine Sungura-WAMJW
Waziri wa Wizara ya afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto, Ummy Mwalimu amesema wizara yake itaendelea kusimamia na kuboresha huduma ya afya kwa kuongeza vituo vya kutolea huduma hadi ngazi ya jamii.
Waziri huyo alitoa kauli hiyo Jumamosi wakati
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
kwenye hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Ummy amesema wizara inatekeleza mpango wa
maendeleo ya afya ya msingi(MAMM) ya kujenga zahanati kila kijiji,vituo vya
afya kwenye kila kata na hospitali kila wilaya.
Aidha amesema wizara inalojukumu la kusimamia sera
ya afya, wataongeza watumishi wa afya
kwa kuongeza udahili wa wanafunzi katika vyuo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment