Na Paul Christian, Ulyankulu.
Paroko wa Parokia ya Kanisa Katoliki Ulyankulu padri
Antony Leonard Katoba amesema eneo lilipojengwa Kanisa Katoliki barabara ya 13
Ulyankulu,mkoani Tabora ni la kihistoria kwa kuwa ndipo ilipokuwa Ikulu ya pili
ya Mtemi Milambo.
Amesema Ikulu hiyo ya Mtemi Milambo ilijulikana
kwa jina la Iselamagazi na ilianza kujengwa mwaka 1879 na kukamilika mwaka
1883.
Padri Katoba anabainisha kuwa Ikulu hiyo ya
Iselamagazi ilitumiwa na Mtemi Milambo kiutawala na pia ilikuwa kambi ya jeshi
la Mtemi Milambo lililojulikana kama “Walugaluga”.
Aidha Paroko huyo ameeleza kuwa Mtemi Milambo
alikuwa na Ikulu nyingine Ikonongo ambapo ndipo yalipokuwa makazi ya Mtemi huyo
mashuhuri.
Padri Katoba anasema, “Mtemi Milambo alianza
kuijenga Ikulu ya Ikonongo mwaka 1880 na kuikamilisha mwaka 1883.”
Paroko huyo wa Parokia ya Ulyankulu amesema Kanisa
Katoliki lilikabidhiwa eneo hilo mwaka 1975 kwa ajili ya kulilinda na kulitunza
na kwamba wanaendelea kulitunza na kulienzi.
No comments:
Post a Comment