Ramadhan
Faraji,Tabora.
Timu
ya soka ya maafande wa JWTZ Rhino Rangers ya mjini Tabora Jumanne imewaondoa maafande
wa Polisi Tabora kwenye michuano ya kombe la Shirikisho kufuatia ushindi wa
mabao 4 kwa 2.
Mechi
hiyo iliyozikutanisha timu hizo inajulikana kama Derby ya mji wa Tabora
ilichezwa kwenye uwanja wa Ally Hassan Mwinyi na kushuhudiwa na mashabiki
wengi.
Iliwachukua
dakika 10 za mchezo maafande wa Rhino Rangers kupata bao la kuongoza kupitia
kwa mchezaji wake Emmanuel Noel ambapo dakika 5 baadae Polisi Tabora walipata
goli la kusawazisha kupitia kwa mchezaji Lucas Patrick.
Timu
hizo ambazo zinashiriki ligi daraja la Kwanza nchini zilikamilisha dakika 90 za
mchezo zikiwa zimefungana bao 1 kwa 1.
Mwamuzi
wa kati Ferdinand Machunde akaamuru kupigwa kwa mikwaju ya penati ili mshindi
apatikane na kusonga mbele katika michuano hiyo.
Kwenye
upigaji wa mikwaju ya penati Rhino Rangers ilipata penati ya kwanza kupitia kwa
Masungu Julias ambapo mpigaji wa Polisi Tabora Michael Chinedu alipoteza mkwaju
wake.
Wachezaji
wa Rhino Rangers waliofunga penati zao
ni Salum Maji na Imani Mwangasora huku Benedict Solomon akikosa penati yake,
kwa upande wa Polisi Tabora aliyefunga penati ya pekee ni Ahamed Mkweche, huku Mohamed Jimngo na Said Shabani wakipoteza
penati zao.
Mwamuzi
huyo wa kati Machunde akisaidiwa na Nestory pamoja na Aswire Faresi akamaliza mtanange
huo kwa Rhino Rangers kuibuka ushindi wa jumla ya magoli 4 kwa 2 ya Polisi Tabora.
No comments:
Post a Comment