Wagonjwa wa wodi tano za hospitali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete
wamesherehekea sikukuu ya Krismasi pamoja na kikundi
cha wanamtandao kijulikanacho ‘Tabora Ndiyo Kwetu’ kwa kuwapelekea
vinywaji, viburudisho, sabuni na mafuta.
Kikundi hicho kiliwafariji wagonjwa hao waliolazwa kwenye wodi hizo kwa kuwapatia vinywaji aina ya
juisi, biskuti, sabuni za kufulia na mafuta ya kupaka.
Mwenyekiti wa Tabora Ndio Kwetu Alexander Ntonge alisema bado wanaendelea
kijipanga ili waweze kutoa msaada mkubwa ambao utawanufaisha wagonjwa
watarajiwa na wao wakiwemo kwani hakuna binadamu aliye kamilika.
Alisema kikundi hicho kilianzishwa
agosti 2014 kikiwa na lengo la kujishughulisha na shughuli za
kijamii na hadi sasa kina wanachama 90.
Mwenyekiti huyo alisema mapema mwezi uliopita baada ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John P. Magufuli kuamua taifa kufanya usafi walimuunga mkono kwa
kufanya usafi kuelekea siku ya Uhuru Disemba 9,mwaka huu katika hospitali
hiyo ya Kitete.
No comments:
Post a Comment