Na
Paul Christian, Tabora.
Rais
wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli ni miongoni mwa Viongozi Mashuhuri
waliozaliwa mwezi wa Oktoba, ambapo alizaliwa tarehe 29.10.1959, Rais wa Rwanda
Paul Kagame alizaliwa tarehe 23.10.1957, Rais wa Kenya Uhuru M. Kenyatta naye
alizaliwa tarehe 26.10.1961.
Rais
wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ambaye ni mwanamke wa kwanza barani Afrika
kushika wadhifa wa Urais alizaliwa tarehe 29.10.1938 na Rais
wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma alizaliwa tarehe 2.10.1953.
Viongozi
wengine mashuhuri waliozaliwa mwezi wa Oktoba ni pamoja na waziri mkuu wa
Israel Benjamin Netanyahu ambaye alizaliwa tarehe 21.10.1949, Waziri mkuu wa
Uingereza David Cameroon alizaliwa tarehe 9.10.1966 na Rais wa Urusi Vladimir
Putin alizaliwa tarehe 7.10.1952.
Viongozi mashuhuri waliowahi kuongoza nchi
mbalimbali na ambao walizaliwa mwezi wa Oktoba ni pamoja na Rais wa awamu ya
nne wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete aliyezaliwa tarehe 7.10.1950, Rais wa
kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta alizaliwa
tarehe 20.10.1891 na Rais Joaquim Chissano wa Msumbiji aliyezaliwa tarehe 22.10.1939.
Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher "iron lady" ambaye
anashikilia rekodi ya kushika wadhifa huo kwa muda mrefu zaidi (1979-1990) na
akiwa mwanamke pekee kushika wadhifa huo alizaliwa tarehe 13.10.1925.
Viongozi wengine Mashuhuri waliozaliwa mwezi wa
Oktoba na kupata kutawala ni pamoja na Rais wa 39 wa Marekani Jimmy Carter
aliyezaliwa tarehe 1.10.1924, Rais machachari wa Iran Mahmood Ahmednejad
alizaliwa tarehe 28.10.1956 na Mahatma Gandhi kiongozi wa vuguvugu la kudai uhuru
na baba wa taifa la India alizaliwa tarehe 2.10.1869.
Watu wengine Mashuhuri waliozaliwa mwezi wa Oktoba
ni pamoja na Graca Machel mwanamke aliyewahi kuolewa na Marais wawili kwa
nyakati tofauti ambao ni Samora Machel wa Msumbiji na Nelson Mandela wa Afrika
Kusini alizaliwa tarehe 17.10.1945 na tajiri maarufu duniani Bill Gates
alizaliwa tarehe 28.10.1955.
Wengine ni Roman Abramovich mmliki wa klabu ya
Chelsea ya Uingereza alizaliwa tarehe 24.10.1966, mwanasoka mashuhuri wa
Agerntina Diego Maradona alizaliwa tarehe 30.10.1960, mcheza soka maarufu wa Brazil
Edison Arantes do Nascinanto “PELLE” alizaliwa tarehe 23.10.1940 na mwanamziki
mashuhuri wa bongo fleva Diamond alizaliwa tarehe 2.10.1989.
Mchezaji maarufu wa klabu ya Manchester United Wayne Rooney alizaliwa tarehe 24.10.1986.
Watu mashuhuri waliozaliwa mwezi wa Oktoba na
nyota zao kung’aa katika chaguzi za kuwania uongozi ni pamoja na Seif Sharrif
Hamad katibu mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF na mgombea Urais wa serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar katika uchaguzi uliofutwa wa Oktoba 25, 2015 alizaliwa
tarehe 22.10.1943.
Katibu mkuu wa zamani wa Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo CHADEMA aliyegombea Urais wa Tanzania mwaka 2010 Dr. Willbrod P. Slaa alizaliwa tarehe 29.10.1948 na mke wa Rais wa 42
wa Marekani Hillary Clinton ambaye anawania Urais wa nchi hiyo kwa tiketi ya
Chama cha Demokratic alizaliwa tarehe 26.10.1947.
Viongozi mashuhuri waliofariki mwezi wa Oktoba ni
pamoja na Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
aliyefariki dunia tarehe 14.10.1999,Rais wa kwanza wa Msumbiji Samora Mashel
aliyefariki tarehe 19.10.1986 na Rais wa kwanza wa Uganda Milton Obote
aliyefariki tarehe 10.10.2005.
No comments:
Post a Comment