Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, December 6, 2015

HOTUBA YA KWANZA YA MBUNGE WA ULYANKULU JOHN P. KADUTU BAADA YA KUAPISHWA


Na Paul Christian, Tabora.


HOTUBA YA MH. JOHN PETER KADUTU MBUNGE WA ULYANKULU ALIYOITOA TAREHE 28 NOV, 2015 KWENYE VIWANJA VYA KANISA KATOLIKI PAROKIA YA ULYANKULU BARABARA YA 13.


Ulyankulu Oyeeeee!!!!
 
We DJ usije kuleta maneno hapa.Najua watu wanataka nipige show, naweza nikapiga hapa ikawa shida.

Mheshimiwa mwenyekiti wa CCM wa wilaya Mzee wetu, mzee Kaseko, 

Mheshimiwa Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa kaka yangu Professor Kapuya,

Wajumbe wa kamati ya siasa wa mkoa wa wilaya,

Waheshimiwa Madiwani wenzangu,

Waheshimiwa Wazee, Vijana, Kinamama na Akinamama,

Mtumsifu Yesu Kristo, Asalam Aleykhum.

Kwanza nimshukuru mwenyezi mungu kutufikisha leo, siku nzuri, siku tuliyovumilia pamoja na mvua. Tunamshukuru sana Mwenyezi Mungu.

Lakini niwashukuru wananchi wote kwa kufika, tena kwa uvumilivu mnanionyesha mnanipenda kweli kweli na mimi ninaona nina deni Bado.Nawashukuruni sana.

Lakini pia niishukuru familia ya mtemi Milambo, jamani leo nimekabidhiwa jambo hili kubwa niko vizuri hapa ukileta mambo ya Ndumba Nangai nakushughulikia.

Mkitaka turudi kwenye uchaguzi nitumie Ndumba Nangai za Milambo mtapata shida,wale watoto wa mama mdogo. 

CCM Oyeeeee!!!!!! Ulyankulu Oyeeee!!!!!

Wazee wangu nawashukuruni sana kwa kunipa heshima, ni heshima kubwa, inayohitaji kuwatumikia wanaUlyankulu kwa moyo thabiti.

Ndugu zangu wanaUlyankulu, Niwashukuru kwa imani kubwa mlioionyesha wakati wa uchaguzi mkuu.Mmenipa nguvu, ushindi wa asilimia 75 na ushee si haba.

Lakini pia ushindi aliopata mheshimiwa Magufuli kwenye jimbo letu ni wa kujivunia,kama sio wa kwanza kimkoa basi wa pili kimkoa,Ninaimani ni wa kwanza kimkoa.Sijawasikia wengine,hii ni jinsi gani imani tuliyonayo. 

Mheshimiwa Magufuli amepata asilimia za kitaifa 58 za kwetu 81 na ushee kwa hiyo utaona tuliochangia kuifikisha 58 mojawapo ni Ulyankulu.Tupaswa kujipongeza sana.

Lakini kwa niaba yake,nawashukuruni sana kwa jambo hilo,pia niwashukuru wapiga kura wote wa jimbo letu kwa kuwachagua madiwani, tena wote wa Chama Cha Mapinduzi.

Kwenye jimbo letu madiwani wote asilimia 100 ni wa Chama Cha Mapinduzi. Kwa hiyo mchango wetu kwenye Halmashauri ya wilaya ya Kaliua, sisi tunatoka tukiwa asilimia 100.Nawashukuruni sana kwa imani hiyo.

Mmekionyesha Chama kokote hadi ngazi ya Taifa kwamba chama cha Mapinduzi kinaaminiwa. Asanteni Sana.

Ndugu zangu uchaguzi umekwisha, na ndio maana leo hapa hatusemi semi vijembe.Ndio maana nimewaambia leo sipigi SHOW.

Maana yake wakati wa Uchaguzi kuzitafuta kura, ilibidi nipige show ili watu waone kama tuko vizuri. Ulyankulu Oyeeeee!!!!!!!!!!!!!!

Uchaguzi umekwisha na sasa kazi tu. Jimbo letu la Ulyankulu tunahitaji kukimbia, nilikuwa nikiiwaambia wakati wa kampeni tunataka maendeleo ya haraka, tunautaka mchakamchaka.
Kwa bahati njema, wananchi wa jimbo letu la Ulyankulu ni wachapakazi. Sasa baada ya kuwa na jimbo tusirudi nyuma,tukadhani jimbo litafanya kila kitu.Niwasihi na niwaombe sana ndugu zangu wa Ulyankulu sasa tuchape kazi kweli kweli.

Tuchape kazi ili maendeleo yetu ya jimbo hili la Ulyankulu yaende haraka haraka.Na hasa kwa kuwa tuko mbioni kutafuta Wilaya na Halmashauri,ili mambo haya yatakapo tufikia twende mbio. 

Tunahitaji uchumi uwe mzuri ndani ya jimbo letu.Tunahitaji kuboresha maisha ndani ya jimbo letu.

Tunahitaji kuboresha huduma za afya.Tunahitaji Elimu, miundombinu ya barabara na mawasiliano.

Lazima tufanye kazi.Lakini ndani ya Ulyankulu ya Makazi kazi nyingi zilifanywa na UN, baada ya kuwa mmepata uraia ndugu zangu sasa kazi.

Kwingine kote maendeleo yanaletwa na wananchi wenyewe,hivyo tuanze kubadilika sasa kujua kwamba tunahitaji kuchangia maendeleo  kuanzia vijiji, kata na hadi kupata wilaya.
Lazima tuhakikishe tunafanya kazi kwa maana ya kuchangia Maendeleo,ili jimbo letu liwe mstari wa mbele na maendeleo yake yaonekane.

Nawajua watu wa Ulyankulu,sisi sio wavivu, niwachapa kazi. Tuongeze kilimo cha tumbaku. Huko nyuma SES kwa maana ya ushuru wa Tumbaku ndani ya makazi haukuwa unarudi kusaidia maendeleo, kwa hiyo sasa tuongeze juhudi kwa kilimo cha tumbaku, pamoja na shida zake.

Tulisema wakati wa kampeni tunaungana wabunge wote wa mkoa, tuhakikishe tunashughulika na zao la Tumbaku ili liboreshwe, ili mapato yajulikane, pembejeo zije kwa wakati.

 Lakini masoko yawepo, bei ziboreshwe, kazi hiyo wabunge wenu wa mkoa wa Tabora tutaifanya muda si mrefu.

Tunataka masoko ya Tumbaku angalau mawili kwa mwezi,sio soko moja kwa miezi miwili, mitatu.

Hatutaki fedha za Tumbaku zije wakati masika imefika.Tunataka fedha ya Tumbaku ije mapema. Lakini tunataka usimamizi wa zao kwa ujumla tushughulike nao.
Kwa hiyo tutaongea na wenzetu wa Ushirika, Bodi ya Tumbaku, na wadau wote wanaohusika na Tumbaku. 

Kwa nini nalisema hili.

Tumbaku ndio zao linaloingiza fedha za kigeni katika mazao ya kilimo.Lakini Tumbaku hiyo hiyo inatoka nyingi Ulyankulu. Lazima tumbaku itusaidie kuboresha maisha yetu.

Ulyankulu Oyeeeee!!!!!!!!!!!!!!

Kwa hiyo ndugu zangu nataka tuongeze spidi ya kilimo lakini juu ya mazao mengine mahindi, maharage, alizeti idara ya ushirika itatusaidia.

Na nina uhakika muda si mrefu mashine za kukamua alizeti zitapatikana.Alizeti, wenzetu wa Singida sasa ni zao linalowasaidia na maisha yanakwenda  pamoja na kwamba eneo lao linaukame.

Lakini kama nilivyosema,ahadi nyingi tumezitoa ni ahadi za miaka mitano.Baada ya kumaliza uchaguzi kumekuwa na shida, watu wakaanza kufikiri kesho yake tu, tunaanza kutekeleza  ahadi, kuna watu wakaanza kuniuliza ulisema maji mbona hatujaona hata mitambo.

Jamani ahadi hizi ni za miaka mitano, tutajitahidi, serikali kwa upande wake itafanya inaloweza. Lakini ziko ahadi za mbunge tutatekeleza moja baada ya nyingine, na tumeanza kutekeleza.

Tumeanza kutekeleza, nikuaambieni ikifika mwaka wa nne nataka asilimia 95 ya utekelezaji wa hizi ahadi uwe umefanyika.

Nikuambieni mimi ni kazi tu. Na tumeanza.

Shida za maji tutahakikisha tunalifanyia kazi, barabara tutafanyia kazi, ziko kazi za binafsi, ziko kazi zitafanywa na TANROAD, ziko kazi zitafanywa na Halmashauri.
Tunauhakika baada  ya miaka mitano serikali ya Chama Cha Mapinduzi itakuwa imetekeleza.  

Bila shaka kila mmoja amesikia kazi imeanza huko, watu wanafurushwa sasa , eeeh ukizubaa kesho anakuja anaibuka tu, ziara ya ghafla na mimi nitazifanya ziara za ghafla.

Nataka nitume salamu kwa watumishi ndani ya jimbo letu, mpo mnanisikia, watumishi wote ndani ya jimbo tunataka kazi,achaneni na siasa,tunataka mtufanyie kazi. 

Mtoe huduma kwa wananchi kwa wakati. Kwa sababu sisi wengine tutafanya kazi mashambani, kila sehemu biashara,tunataka wafanyakazi ndani ya jimbo letu wafanye kazi inayoonekana. 

Na tutaiagiza serikali. Alikuwepo hapa mkuu wa wilaya, alikuwepo Mkurugenzi.Tunataka wafanyakazi wa jimbo letu wachapekazi. Sio kuwa mwanzo wa matatizo,  sio kukaa vijiweni,sio kushughulika na siasa.Siasa tuachieni akinaKadutu na wengine.

Ulyankulu Oyeee!!!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa hiyo ndugu zangu, leo sherehe yetu hii ilikuwa ni kujipongeza lakini kuanza kuona kwamba tunataka kufanyanini. Tunayo mambo mengi mno ya kufanya.Lakini jambo moja niwaambie basi.

Ndio maana niliwaambia sisi utekelezaji unaanza mara moja tumefuatilia na baadae tumefanikiwa, kusajili kata tatu za Ulyankulu. Nilikuambieni niachieni mi ndio najua njia.
Tumeisha pata kata tatu, sasa tunaisubiri tume ya uchaguzi itapanga utaratibu wa uchaguzi, ndani ya kata zetu tatu za ulyankulu. 

Lakini ninauhakika tutaendelea kuomba kata ziongezwe hasa eneo hili la Makazi Ulyankulu ili tuwe na kata nyingi za kutosha.

Ni imani yangu tukipata kata mambo yatakwenda vizuri.

Ulyankulu Oyeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!

Kwa hiyo ndugu zangu muda na wenyewe umetutupa hatuna maneno mengi zaidi ya kuwashukuru lakini nataka kukuambieni tumeisha anza kazi na nitapita kijiji kwa kijiji, kuhakikisha ahadi ambazo tumezitoa tunaanza kutekeleza.

Kuna ahadi kwa mfano tumetoa kwa ajili ya mifuko ya simenti ya zahanati, tunaanza Disemba hii kutoa simenti kwa zahanati.Nia yetu ni kuhakikisha watu wanapata huduma ya afya ili kazi za maendeleo zifanyike na kadhalika.

Lakini kabla sijamaliza nimshukuru kwa dhati kaka yangu Professor Kapuya, kwa dhati kabisa, Profesor amekuwa msaada kwangu kabla ya kupata ubunge na sasa na hata leo mnavyomuona hapa ametoka Dar es Salaam kwa ajili ya shughuli hii tu.
Akimaliza hapa anarudi zake Dar es Salaam. 

Eeeeee huyo ndio Kapuya bwana.Nimelisema hili, kaka yangu ameanza kunisaidia mnayo habari tumekwisha kuanza vikao vya bunge,Keisha anza kunionyesha njia ukienda pale, yule atakusaidia, ukienda kwa huyu katibu atakusaidia.
 kazi hiyo Kapuya keisha anza kuifanya. Na nimeanza kuwa mwenyeji bungeni.

Ulyankulu Oyeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Eee unajua ukikuta wenyeji wazuri, basi huimgeni,mambo yanakwenda vizuri. Lakini niseme tena SITAWAANGUSHA. Januari tunaanza shughuli mtaishuhudia.
Ulyankulu Oyeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Si mnaijua, nataka kuwa king’ang’anizi huko, nyie muda ukifika kaeni huko muwe mnachungulia,halafu shughuli itakuja.

Ndugu zangu naomba niwatambulishe sasa, Lufungija njoo,Chatanda ukae, huyu afisa tarafa alitaka kuacha kazi yake awe katibu wa mbunge, sasa nimemwambia yeye akae tu.
Jamani huyu mdogo wangu mheshimiwa Jafael Lufungija ndiye katibu wa mbunge kuanzia leo. 

Huko nyuma alikuwa anaratibu, sasa leo kulitokea mkanganyiko kati ya afisa tarafa na  yeye, nani katibu wa mbunge, sasa huyu ndio katibu wa mbunge.

Kamati ya kampeni, sijui mpo, kamati ya kampeni ya Jimbo Asante, lakini kipekee nimshukuru mdogo wangu mheshimiwa Kitogoli diwani mstaafu upo!!!

La mwisho ndugu zangu watu wa Ulyankulu zipo alama za ubaguzi, zipo alama za ubaguzi, naomba tuzikemee kumekuwepo na dalili za ubaguzi watu wanasema huyu Msukuma, huyu Mnyamwezi, huyu Mhutu. 

Naomba Tuzikemee.Tunataka kuijenga Ulyankulu yenye umoja, Ulyankulu isiyokuwa na ubaguzi.

Huyu ndio mheshimiwa Kitogoli tulipambana hapa wakati wa kampeni ….. Ah maneno mengi sana huyu.


Eeh huyu tulikuwa tunamtanguliza wakati wa kampeni anapiga, anapambana na yale maneno yakifedhuli fedhuli. Na siku nyingine nitamleta, Nimeshaona ni dawa. 

Lakini nataka niwakumbushe baada ya uchaguzi kwisha madiwani walioshinda, mbunge wenu, na Rais ni viongozi wanawatumikia wananchi wote,bila kujali itikadi.

Niwakaribishe sana ndugu zangu wa CHADEMA, CUF, ACT tuungane kwa ajili ya maendeleo ya Ulyankulu. Itikadi zetu tuziweke pembeni kwa sababu ya maendeleo. 

Baada ya kusema hayo ndugu zangu naomba nifanye kazi moja. Mimi ni mtu wa michezo kila nilimotembea niliahidi kutoa jezi pamoja na mipira.

Leo ninayomafurushi yako kwenye lori pale.Vijiji vyote vinapata jezi na mipira. HAPA KAZI TU.

Ulyankulu yote itavaa jezi mpya na mipira mipya. Tumeanza na michezo. Lakini muda si mrefu mtaona tunashughulika na visima, tunashughulika na maji kabla ya serikali kuleta pesa.

Tunataka kutumia hizi hizi posho, posho hizi hizi za Mbunge zianze kufanyakazi kabla ya pesa ya serikali haijaja. Pesa ya serikali itatukuta tupo njiani tunaendelea, ndio kazi ya maendeleo hatutaki bla bla.

Tunataka tuwe mbele kuliko wengine. Na ninaimani nikuambieni Halmashauri inakuja, Wilaya inakuja na niwadokeze Mheshimiwa Majaliwa lilipotajwa jina lake tunaelekea kupiga kura kumpitisha Bungeni nilinong’onezana naye. 

Basi hizo ndio kazi zangu kupenya.Lazima uwe na kiongozi mjanja. Nimezaliwa Ichemba lakini mimi mtoto wa mjini.

Ulyankulu Oyeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!

Mheshimiwa Majaliwa alikubali, atakuja siku moja kutembea Ulyankulu. Tuendelee kumuombea kazi ni nzito ile, lakini iko hazina moja kwa mheshimiwa Majaliwa anayajua maeneo yote alivyokuwa Urambo pamoja na Ulyankulu. 

Tena akaniuliza barabara ya 13 pakoje, nikamwambia pamechangamka sana siku hizi.

Ulyankulu Oyeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!

Sasa ndio salamu tunaendelea kupenya siku moja nitawaambia tumepenya vipi. Kazi yangu itakuwa kuleta taarifa hapa za bungeni kabla na baada.

Tutatafuta utaratibu ili mjue tunafanya nini na tutatoa taarifa kila wakati kwenye mikutano ili kila mwananchi ajue.

Lakini jambo lingine ni juu ya Chama Chetu cha Mapinduzi, lazima tukiimarishe chama chetu cha Mapinduzi kwa ajili ya uchaguzi ujao wa mwaka 2020.

Lazima tuhakikishe tunajenga ofisi za matawi na kata kwenye maeneo yetu. Hiyo tutakuwa tumeimarisha chama chetu kiwe imara tusipate tabu.

Lakini kubwa nimeisha zungumza na katibu wa wilaya dada yangu Neema Adamu anatayarisha utaratibu wa kuja kutoa semina kwa viongozi wote wa Matawi.

Mtakula na kulala ili watu wajue shughuli za chama zikoje.Tulipata tabu kidogo wakati wa Kampeni kukawa na shida watu hawajui hata hitifaki.

Sasa tunataka kuleta mafunzo kwa viongozi wote wa Matawi pamoja na Mabalozi ili kuhakikisha kila mmoja anajua wajibu wake lakini ili uchaguzi ujao wa mwaka wa 2020 tusipate tabu.

Tunataka 2020  Mbunge apate asilimia 99.9, Rais apate asilimia 100.
Najua kazi kubwa tuliyoifanya wenzetu wale waliondoka saa tisa za usiku kabla ya matokeo, tunajiandaa kwa mwaka 2020 kimbunga hicho kitakuwa kikali kuliko hiki.

Ulyankulu Oyeeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!

Sasa waheshimiwa wananchi pamoja na viongozi nimalizie kazi hii, hii ni sampuli mafurushi yako kwenye lori.

Nimuombe  diwani mtarajiwa wa Milambo aje hapa halafu mbunge mstaafu atakuwa akiwapatia seti ya jezi.

Tabu tuliyonayo mbunge huyu mstaafu anamatatizo yeye ni Simba sana, sasa ameamua kumchagulia Moleka Jezi Nyekundu……………. Hivi vingine na Mpira utamuona katibu wa Mbunge.

Anayefuata diwani mtarajiwa wa Igombemkulu na diwani mtarajiwa wa Kanindo awe karibu, naomba mwakilishi wake.

Mwakilishi, Sasa upendeleo nani apewe, Haya Seleli, diwani wa Seleli mheshimiwa Buyobe. …………………….Tatizo anataka kuacha kugawa sababu ni za Yanga. 

Jamani hii ni Sampuli, mzigo huko kwenye Lori pale, vijiji vyote vinapata, sawa!!!!

Lakini wakati huo huo tukijiandaa baada ya masika kuna mashindano yanakuja lakini kwa wakati huu nimekwisha zungumza na uongozi wa chama cha Mpira mkoa wanatuandalia wakufunzi wakuja kufundisha kwa ajili ya makocha pamoja na waamuzi wa Mpira.

Baada ya kusema hayo niwashukuru tena, nawashukuruni kwa kuja lakini kubwa nawashukuruni kwa kuniamini. 

NARUDIA SITAWAANGUSHA NDUGU ZANGU, ASANTENI SANA NA MBARIKIWE SANA, ASANTE.



No comments: