Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Wednesday, December 9, 2015

KAYA 12,300 ZANUFAIKA NA MRADI WA MIYOMBO UYUI

Na Halima Ikunji,Tabora

JUMLA ya kaya 12,300 zimenufaika na mradi wa msitu wa Miyombo katika vijiji 42 ambavyo vinazunguka eneo la msitu huo wenye hekta 306.6 uliopo  wilaya ya Uyui mkoa wa Tabora.
  
Akisoma taarifa fupi katika eneo mradi huo mbele ya Mkurugenzi mkazi wa Umoja wa Mataifa  Alvaro Rodrigues mmoja wa wafugaji nyuki Baraka Moshi alisema chama chao cha wafugaji nyuki, Mbola Mashariki kilianzishwa mwaka 2012 kikiwa na wanachama 10  hadi kufikia sasa  kina wanachama 190 kati yao wanaume 173 na wanawake 17.
  
Alisema kwa sasa wana mizinga ya nyuki  5,375 kati ya hiyo 5,000 ni mizinga ya kienyeji na 375 ni ya kisasa .

Moshi alibainisha kuwa mizinga 4,700 ina nyuki na mizinga 300 haina nyuki kwa mizingi ya kienyeji ambapo kwa upande wa mizinga ya kisasa 60  haina nyuki.

Akizungumzia malengo ya ufugaji wa nyuki alisema ni kuhifadhi  na kutunza mazingira na kujipatia kipato kwa kuuza asali na nta.
  
Moshi alisema lengo la kikundi hicho ni kuhakikisha kuwa msitu wa Mbola unakuwa na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho kwa kufanya usimamizi endelevu wa kutovamia msitu kwa lengo la kuchoma mkaa na kupasua mbao bila utaratibu.


Aidha alieleza changamoto walizonazo ni  ukosefu wa jengo la usindikaji, mashine za kisasa za usindikaji pamoja  na kutokuwa na masoko ya uhakika kwa bidhaa wanazozalisha.


Alitaja changamoto nyingine ukosefu wa bwawa la maji kwa ajili ya umwagilia wa bustani za mboga mboga na mashine na kusindikia matunda.


Kwa upande wake kaimu Mratibu wa Miyombo mkoani Tabora, Yobu Kiungo alisema Lengo la mradi huo wa miombo ni kutunza baiyoanuai ya misitu ya Kongo iletayo mvua ukanda wa kati wa Afrika na  uhifadhi wa mazingira.

Alifafanua kuwa lengo mahususi la mradi huo ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya biashara na chakula ili kuongeza kipato kwa wananchi wanaozungukwa na mradi wa miyombo katika maeneo ya vijiji 28 vya wilaya ya 4 zilizopo Mkoa wa Tabora na Katavi ambazo ni Uyui, Urambo, Kaliua na Mlele.
  
Kwa upande wake mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodrigues, alisema wanataka kuona thamani ya miradi inaendana na fedha zinazotolewa.










Reply Reply to All Forw

No comments: