Na Paul Christian, Tabora.
Mtemi Milambo alizaliwa mwaka 1820 eneo
lililojulikana kwa jina la Ikonongo na alipewa jina la Mbula Kasanda.
Baba yake mzazi na Mtemi Milambo aliitwa Kasanda na
mama yake alijulikana kwa jina la Mwasi Mpela.
Babu yake na Mtemi Milambo aliyejulikana kwa jina
la Kasele Muhofu na ambaye aliishi miaka 300 baada ya kuzaliwa mwaka 1520 na
kufariki mwaka 1820 alimrithisha utemi mjukuu wake Mbula Kasanda (Milambo).
Babu yake Mtemi Milambo, Kasela Muhofu kwa maajabu
aliongea akiwa tumboni mwa mama yake kabla ya kuzaliwa na baada ya kuzaliwa
hakunyonya maziwa ya mama yake.
Mbula Kasanda (Mtemi Milambo) kabla ya kutawazwa
kuwa mtemi alitanguliwa na watemi tisa wa kwanza akiwa Sibuga aliyetawala
kuanzia mwaka wa 22BK akafuatiwa na Mkindo wa Kwanza ambaye alirithiwa na Mlowa
na kisha kufuatiwa na Moto wa Tatu.
Moto wa Tatu alirithiwa na Nsimba Nchembe ambaye
naye alimwachia utawala Kapaya aliyerithiwa na Kasele Muhofu ambaye alimuachia
utawala Kasimana Kasele.
Kasimana Kasele alikabidhi utawala kwa Mkindo wa Pili
ambaye alimrithisha Mbula Kasanda maarufu kama “Mtemi Milambo.”
Mtemi Milambo alianza kutawala mwaka 1838 katika
eneo la Ikonongo huku akiwa na Ikulu mbili za Ikonongo na Iselamagazi.
Kabla ya kifo chake kilichotokana na homa kali, Mtemi
Milambo aliacha urithi wa kiti cha utemi kwa mtoto wake wa kike aliyejulikana
kwa jina la Kibete mnamo mwaka wa 1884.
Kibete alizaliwa akiwa na ziwa moja yaani "titi
moja" la mkono wa kushoto.
Kabla ya Kibete kufariki alikabidhi kiti cha utemi
kwa Solomoni Kazwika Milambo ambaye alizaliwa siku ya Jumatatu asubuhi ya tarehe
18 Julai, 1945 ambaye yupo hadi hivi sasa.
Solomoni Kazwika Milambo kabla ya kuzaliwa
aliongea akiwa tumboni mwa mama yake na hakunyonya maziwa ya mama yake.
No comments:
Post a Comment