
Na Paul Christian, Tabora
Magoli yaliyofungwa kipindi cha
kwanza na washambuliaji Dario Benedetto na Martin Zuniga yameiwezesha Timu ya
Club America ya nchini Mexico kuibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya
Mabingwa wa Vilabu Barani Afrika TP Mazembe yenye masikani yake Lubumbashi,
Congo DR.
Dario Benedetto ndiye aliyekuwa wa
kwanza kufumania nyavu za TP Mazembe katika dakika ya 19 ya mchezo baada ya
kuunganisha kwa kichwa kross iliyochongwa kutoka winger wa kushoto Paul
Aguilar.
Mabingwa wa vilabu barani Afrika TP
Mazembe walipata bao lao la kufutia machozi kupitia kwa Rainford
Kalaba.
Kocha
wa TP Mazembe Patrice Carteron amesema timu yake
ilikuwa kwenye kiwango kizuri mwishoni mwa ligi ya mabingwa barani Afrika ingawa
walipofika Japan walikuwa na siku tatu za maandalizi kabla ya kucheza mechi yao
ya kwanza.
“Tungepata angalau siku 10
zingetosha kutuweka fiti zaidi kiushindani na kutokana na hali hiyo hatukuwa
katika hali ya kucheza mechi ya ufunguzi kwa ushindani.”amesema kocha huyo TP
Mazembe.
Mechi hiyo ya kusaka nafasi ya tano
katika michuano ya Kombe la Dunia kwa ngazi ya mabingwa wa vilabu katika Mabara
ilichezwa leo kwenye uwanja wa Osaka Nagai nchini Japan.
Kocha wa Club America iliingia
uwanjani akiwa amejeruhiwa baada ya kupoteza mechi ya nusu fainali katika
dakika za mwisho za mchezo mbele ya Guangzhou Evergrande wakati kocha wa TP
Mazembe Patrice Carteron aliingia uwanjani akiwa na nia ya kuonyesha matumaini
baada ya kupoteza mechi yao kwa mabao 3 kwa 0 kutoka kwa Sanfrecce Hiroshima.
Ingawa makocha wote wameshuhudia
vijana wao wakicheza mchezo mzuri ni dhahiri kuwa kocha wa Club Americana,
Ambriz anakwenda nyumbani akiwa mwenye furaha zaidi.
No comments:
Post a Comment