Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Thursday, December 10, 2015

DR.MAGUFULI:ATANGAZA BARAZA LA MAWAZIRI




Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dr John Pombe Magufuli ametangaza Baraza la mawaziri wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania.

Hotuba ya Dr.Magufuli: Kumekuwa na speculation nyingi na watanzania wamekuwa na hamu kubwa ya kujua Baraza la Mawaziri, baada ya kusubiri kwa muda mrefu, baada ya kuapa tulitakiwa angalau tarehe kumi tuwe tumetangaza Baraza.

Tuliona angalau tujiridhishe kwanza, Baraza lililopita lilikuwa na Mawaziri na Manaibu zaidi ya 59, tukaona tuwe na Baraza dogo.

Hatuwezi kukaa bila Baraza, katika Baraza hili, wizara nyingi tumeziunganisha na kutakuwa na wizara 18 na tutakuwa na mawaziri 19 tu, kuna baadhi ya wizara zitakuwa na Mawaziri na hazitakuwa na Manaibu waziri.

Lengo ni kutimiza ahadi yetu ya kuwa na Baraza dogo kupunguza gharama na effective kwa kufanya kazi.

Zilitengwa bilioni 2, Mawaziri watakapoteuliwa waende semina elekezi.
Baraza nitakaloliteua halitakuwa na semina elekezi na fedha tutaelekeza sehemu nyingine kama ni madawati au kwenye elimu bure.

Watafanya semina elekezi wenyewe ndani kwa ndani.

WIZARA
1.Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Utumishi na Utawala Bora: Mawaziri ni George Boniface Taguluvala Simbachawene na Angellah Jasmine Mbelwa Kairuki, Naibu waziri Selemani Saidi Jafo.

2.Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira: Waziri ni January Yusuf Makamba, Naibu Luhaga Mpina

3.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu: Waziri ni Jenista Muhagama, Manaibu Anthony Mavunde, Possy Abdallah.

4.Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi: Waziri ni Mwigulu Lameck Nchemba, Naibu William Ole Nasha

5.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano: Waziri bado sijamtafuta, naendelea kumfikiria, Naibu waziri mhandisi Edwin Ngonyani.

6. Wizara ya Fedha na Mipango: Waziri bado tunamtafuta, Naibu waziri ni Ashantu Kizachi

7.Wizara ya Nishati na Madini: Waziri ni Professa Sospeter M. Muhongo, Naibu waziri ni Medadi Kalemani

8.Wizara ya Katiba na Sheria: Waziri Dr. Harrison George Mwakyembe

9.Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa: Waziri ni Augustine Philip Mahiga ambae nimemteua kuwa mbunge na kisha waziri, Naibu ni Dr Suzan Kolimba.

10.Wizara ya Ulinzi na Kujenga taifa: Waziri ni Dr. Hussein Ali Mwinyi

11.Wizara ya Mambo ya Ndani: Charles Muhangwa Kitwanga

12.Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi: Waziri ni William Vangimembe Lukuvi, Naibu Angelina Mabula

13.Wizara ya Maliasili na Utalii: Waziri bado, Naibu ni Ramo Makala.

14.Wizara ya Viwanda, biashara na uwekezaji: Waziri Charles John Poul Mwijage

15.Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi: Waziri bado hajapatikana, Naibu ni Stella Manyanya.

16.Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto: Waziri Ummy Ally Mwalimu, Naibu ni Hamisi Andrea Kigwangalla.

17.Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo: Waziri Nape Nnauye, Naibu Anastazia Wambura.

18.Wizara ya Maji na Umwagiliaji: Waziri Makame Mnyaa Mbarawa ambae nilimteua kuwa mbunge, Naibu ni Isack Kamwela.


 

No comments: