Na Ramadhan Faraji, Tabora.
Timu ya Abajalo yenye masikani yake wilaya ya
Igunga mkoani Tabora imeshindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani wa Ally
Hassan Mwinyi baada ya kukubali kichapo cha magoli 3 kwa 1 kutoka kwa Singida
United ya mjini Singida.
Mechi hiyo ambayo ilichezwa Jumapili na kushindwa
kumalizika ndani ya dk. 90 kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mjini Tabora,kabla
ya mwamuzi wa kati kuiahirisha mechi
hiyo Singida United walikuwa wakiongoza kwa mabao 2 kwa 1.
Mechi hiyo iliendelea tena Jumatatu asubuhi kwa
timu hizo kumalizia dk. 22 zilizosalia kabla ya mechi hiyo kuhairishwa siku ya
Jumapili ambapo Singida United waliweza kuzitumia vyema dk hizo 22 kwa kufunga
goli moja na kufanya matokeo kusomeka mabao 3 kwa 1 hadi dakika 90 za mchezo
zinakamilika.
Aidha Ligi Daraja la Pili ngazi ya Taifa imeendelea tena jioni ya siku
ya Jumatatu katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi kwa kuzikutanisha timu za
Milambo FC ya Tabora na Mvuvuma ya Kigoma.
Shukurani zimwendee mchezaji wa Milambo FC Rashid
Kabole aliyeipatia timu yake goli moja la pekee na la ushindi kufuatia
kuukwamisha nyavuni mpira wa penati.
Hadi mwisho Milambo FC watoto wa Nyumbani waliibuka na Ushindi wa
bao moja kwa sifuri dhidi ya wapinzani wao Mvuvuma FC na hivyo kujikusanyia
pointi tatu muhimu.
No comments:
Post a Comment