Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Friday, December 11, 2015

LEOPORD ULAYA: AWA MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA TABORA


Na Hastin Liumba,Tabora


Hatimaye Madiwani wa halmashauri ya Manispaa ya Tabora wamefanya uchaguzi wa  Meya na Naibu  baada ya kuvutana kwa muda mrefu.

Uchaguzi huo uligubikwa na ubishani wa namna ya kupiga kura baada ya mkurugenzi mtendaji wa Manispaa hiyo Zipola Liana kutoa maelekezo ya utaratibu wa kupiga kura kwenye  kizimba jambo lililopingwa na baadhi ya madiwani waliotaka kupiga kura mahali walipokaa.

Hata hivyo afisa wa uchunguzi mwandamizi wa TAKUKURU mkoa wa Tabora Henri Mwankusye alitoa ufafanuzi wa sheria ya TAKUKURU pamoja na ile ya uchaguzi kwa madiwani hao.

Lakini wakati afisa huyo wa TAKUKURU akitoa ufafanuzi wa vifungu vya sheria, baadhi ya madiwani walikuwa wameanza zoezi la kupiga kura huku wakiwa wameketi katika nafasi zao.

Kutokana na hali hiyo mbunge wa Tabora mjini Emmanuel Mwakasaka aliomba mwongozo na kutaka uchaguzi huo uanze upya kwa kuwa tayari dosari imejitokeza kwa baadhi ya madiwani kupiga kura huku wakioneshana.

“Ndugu zangu hapa tumepewa mwongozo na viongozi wetu na tayari kura 17 zimeshapigwa kimsingi tunapaswa tuanze upya kwa kufuata
mwongozo ili tusipate malalamiko ya dosari za uchaguzi huu.’Alisema
Mwakasaka.

Mabishano hayo yalidumu kwa takribani nusu ambapo madiwani waliridhia kupiga kura kwenye kizimba na kutumbukiza kura  kwenye kisanduku.

Vyanzo vya taarifa vimebainisha kuwa baadhi ya madiwani
wa CCM walitaka kuvuruga uchaguzi huo kwa kumpigia mgombea wa CHADEMA Conel Ng`andu kwa sababu wagombe waliowaunga mkono kwenye nafasi ya Umeya kutopitishwa na vikao vya CCM.

Katika uchaguzi huo diwani wa kata ya Mpera Leopord Ulaya wa CCM
alishinda kwa kura 32 dhidi ya mgombea wa CHADEMA Conel Ng`andu wa kata ya Malolo aliyepata kura 8.






No comments: