Na Paul Christian.
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp
Blatter amesema yeye bado ni Rais wa shirikisho hilo licha ya kufungiwa
kujihusisha na masuala ya michezo kwa muda wa miaka minane na kupigwa faini ya
dola za kimarekani 50,000.
Kamati ya maadili ya shirikisho hilo imechukua
hatua hiyo baada ya kubaini Blatter aliidhinisha malipo ya dola za kimarekani
mil. 2 kwenda kwa Rais wa Shirikisho la Soka barani Ulaya UEFA Michel Platini
mwaka 2011 ili asaidiwe kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka huu.
Blatter amesema akiwa Rais wa shirikisho hilo hawajibishwi
na kamati ya maadili ya FIFA isipokuwa mkutano mkuu wa shirikisho hilo ambao
kwa mujibu wa ratiba umepangwa kufanyika mwezi Februari mwaka 2016.
Amesema, “ninaomba radhi, ninaomba radhi kwa ajili
ya FIFA.”
Blatter amesikitishwa na utaratibu uliotumiwa wa
kutoa taarifa za kufungiwa kwake kwa vyombo vya habari kabla ya kutaarifiwa yeye
binafsi.
Aidha kamati hiyo ya maadili ya FIFA imemfungia
Rais UEFA Michel Platini kutoshiriki masuala ya michezo kwa muda wa miaka
minane kutokana na kupokea fedha hizo.
Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 na ambaye
amelitumikia shirikisho hilo kwa miaka 17 anatuhumiwa kwa kupokea hongo,rushwa,
kutoa na kupokea zawadi mambo ambayo yako kinyume na maadili ya FIFA.
Hata hivyo uongozi wake ulikuwa unafikia ukomo
mwezi Februari mwaka 2016 kufuatia kujiuzulu kwake mara baada ya kuchaguliwa mapema
mwaka huu kutokana na tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa.
No comments:
Post a Comment