Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, December 20, 2015

DEREVA WA BASI LA ALLYS STAR ASOMEWA MASHITAKA 22



NA Lucas Raphael,Urambo.

DEREVA wa basi la  Allys Star, Alfa Haji (37) lililopata ajali lilipokuwa likisafiri kutoka wilaya ya Kaliua kuelekea jijini mwanza amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya Urambo mkoani Tabora akikabiliwa na mashitaka 22 ikiwemo kusababisha vifo vya watu wanane na majeruhi 13.

 Akisoma mashitaka hayo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Hassani Momba mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi mkaguzi msaidizi Felibet Pima alisema kwamba mnamo desemba 15 mwaka huu majira ya saa 12 asubuhi katika kijiji cha vumilia wilaya ya urambo mtuhumiwa huyo aliendesha gari kizembe na kupata ajali iliyosababisha vifo vya watu wanane .

Alisema kwamba licha ya kusababisha vifo vya watu wanane pia  alisababisha majeruhi kwa watu 13.

Mwendesha mashitaka huyo aliwataja marehemu waliotambuliwa kuwa ni Hamisi Ramadhani mkazi wa Magiri mkoani Tabora,Grace Andrew(24) mkazi wa Ng'ambo Tabora, Paschal Abdul (miezi 8) mkazi wa Bunda,Tipwege Kataga(20), Emeliana Tryphon(24) , Antoni Julius Mkazi wa Wilayani Kaliua,Shija Anton mkazi wa Kaliua na Rahel Mussa Mkazi wa Ulyankulu wilayani Kaliua.

 Aidha mwendasha mashitaka wa jeshi la polisi ,Pima aliwataja majeruhi mbele ya mahakama hiyo kuwa ni Pili Juma (15),Maro Machano(50),Gift Mayunga(29),Ibrahimu Hasani (25),Rahel Mabula (20)Jane Inosent(29) Anges Michael ,Godlifa Alois (35).

 Wengine ni Santo Lufasiza (28) Mariamu Cosmas (38)Fatuma Juma (19) Yunge Sini (9) na Marthar Luhende (21)

Hata hivyo mtuhumiwa huyo alikana mashitaka yote 22 na amerudishwa rumande  kwa usalama wake na kesi hiyo  itatajwa tena desemba 31 mwaka huu.

No comments: