Na Paul Christian, Tabora.
Pongezi hizo zimetolewa leo na Katibu wa Siasa,
Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Uyui Bwana Said Katala
wakati wa mahojiano maalum na mwandishi wa blog ya Tabora Watch.
Amesema wabunge hao wamesababisha watendaji na
viongozi wa CCM ngazi ya mashina, matawi, kata na wilaya kutekeleza majukumu
yao kwa ari na nguvu mpya baada ya kuwaunganisha kwa kuweka kando tofauti
zilizojitokeza kwenye michakato ya uchuguzi uliopita.
Bwana Katala amebainisha kuwa wabunge hao kwa pamoja
wameweza kuweka rekodi ambapo kwa mara ya kwanza katika historia ya chama wilayani humo wameitisha
kikao cha kazi kilichowakutanisha wenyeviti na Makatibu wa CCM ngazi ya kata,
Madiwani, wajumbe wa sekretariet ngazi ya wilaya pamoja na Kamati ya siasa ya
wilaya hiyo.
Amesema kikao hicho kimewawezesha viongozi hao
kuwa timu moja yenye lengo moja katika kuimarisha chama na kuisimamia serikali katika
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015.
Katibu huyo wa Siasa,Itikadi na Uenezi wa CCM wilaya
ya Uyui amewataka wabunge hao kutokatishwa tamaa na watu wachache ambao
wamekuwa wakitoa maneno ya uzushi kwa maslahi yao binafsi na kwamba wao wachape
kazi tu.
Kikao hicho kilichoitwa “kikao cha kazi”
kiliwahusisha viongozi hao kutoka kata 30 za majimbo ya Tabora Kaskazini na
Igalula wilayani humo ambapo kwa pamoja walitoka na kauli mbiu ya "MAENDELEO KWANZA, MAJUNGU BAADAYE, HAPA KAZI TU."
No comments:
Post a Comment