Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Thursday, December 10, 2015

DC: WATUMISHI WA UMMA WAACHE KUFANYA KAZI KWA MAZOEA



Na Hastin Liumba,Nzega

Watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Nzega mkoani Tabora wameagizwa kuacha kufanya kazi za umma kwa mazoea na badala yake wabadilike ili kuendana na kauli mbiu ya hapa kazi tu.

Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na mkuu wa wilaya hiyo Jackline Liana alipokuwa akihutubia baraza la madiwani wilayani humo.

Alisema wapo baadhi ya watendaji ambao siku zote  hawabadiliki
katika utendaji wao hivyo watendaji wa namna hiyo hawatakuwa na nafasi kuendelea kufanya kazi katika halmashauri hiyo.

Liana aliwaonya watumishi wenye tabia ya  uvivu, utoro,uzembe na wenye visingizio vya ruhusa kila kukicha.

“Una afya njema uliyojaaliwa na Mungu sasa vipi unaomba kazi unapata halafu unashindwa kutimiza wajibu wako, binafsi sitakuwa na mswalia mtume kwa watu namna hiyo.”alisema mkuu huyo wa wilaya.

Alisema taifa ili lisonge mbele kimaendeleo linahitaji watumishi wanaoheshimu muda na kufanya kazi kwa bidii.

Aidha aliwataka madiwani wa halmashauri hiyo kutimiza wajibu wao
kwa wapiga kura ambao waliahidi mambo mengi kuwafanyia baada ya uchaguzi.

Mwenyekiti mpya wa halmashauri hiyo Makula Kiwele alisema hatolea uzembe na kwamba atashirikiana na watumishi wachapakazi kutekeleza majuku yake katika kuharakisha maendeleo ya Nzega.

No comments: