Na Lucas Raphael, Nzega.
MDAU wa elimu
Zakaria Luzwilo wa kata ya Puge wilaya ya Nzega Mkoani Tabora ametoa
Msaada wa madawati 5 yenye thamani ya shilingi 300,000/- kwa shule ya msingi Isunha kwa lengo la kukabiliana na upungufu wa madawati shuleni hapo.
Mdau huyo
ambaye alisoma katika shule hiyo miaka 1980 amesema ametoa madawati hayo ili
kuonyesha mchango wake pamoja na kuhamasisha watu wangine kujitolea kulikabili tatizo hilo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi
madawati hayo kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo Mathew Shija, mdau huyo amesema ametoa msaada huo mdogo ili hamasa kwa
watu wengine kujitolea hata kwa kidogo walichonacho kusaidia sekta ya elimu.
Zakaria amesema mwaka jana
alialikwa na uongozi wa shule hiyo kuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya darasa
la saba na kuhaidi kutoa msaada wa madawati hayo na kwamba ametimiza ahadi
hiyo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya
msingi Shija amemshukuru mdau huyo wa elimu kwa msaada wa madawati hayo ambayo
yatasaidia kupunguza pengo la mahitaji halisi ya madawati shuleni hapo.
Aidha amesema msaada huo ni
mkubwa kutoka kwa mtu binafsi toka alipohamia shuleni hapo mwaka 2000.
Zakaria amempongeza mdau
huyo wa elimu kwa kuonyesha moyo wa kizalendo na fadhila kwa shule aliyosomea.
Mwalimu mkuu huyo
amebainisha kuwa shule hiyo ina wanafunzi 355 na inakabiliwa na upungufu wa
madawati 50 na yaliyopo ni sasa ni 100.
No comments:
Post a Comment