Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Sunday, February 21, 2016

LIGI DARAJA LA TATU: MAAFANDE WA JKT MSANGE WATOKA SULUHU NA TABORA FC "WATOTO WA MJINI"


Na Ramadhan Faraji, Tabora.

Ligi daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Tabora imeendelea Jumapili jioni kwenye uwanja Ally Hassan Mwinyi kwa kuwakutanisha wafunga buti maafande wa JKT Msange na Tabora FC “Watoto wa Mjini.”

Mechi hiyo ilikuwa ya kiufundi zaidi kwa timu zote mbili na mara kadhaa zilionekana kukamiana kwa kutumia nguvu katika ukabaji na ushambuliaji.

Hadi mwisho wa mechi hiyo si JKT Msange wala Tabora FC “Watoto wa Mjini” waliofanikiwa kuona lango la mpinzani wake na hivyo kuufanya ubao wa matokeo kusomeka JKT Msange 0 v 0 Tabora FC.

MSIMAMO WA KUNDI B LIGI DARAJA LA TATU NGAZI YA MKOA.

#
TEAM
PTS
1.
JKT Msange
4
2.
Tabora FC
4
3.
Saba Saba FC
3
4.
Maji Maji FC
0

No comments: