Na Deogratius Yagomba, Tabora.
Timu
ya masumbwi (Ndondi) ya mkoani wa Tabora inayoshiriki kwenye michuano ya
taifa imeendelea kufanya vizuri jijini Dar es Salaam.
Akiongea
kwenye kipindi cha Meza ya michezo katibu na mwalimu wa kikosi hicho Yahaya
Bageleza amewataja mabondia wanaowakilisha mkoa wa Tabora kwenye michuano
hiyo kuwa ni Bakari Athuman, Maneno
Athuman, Musa Haruna na Wami ramadhani.
Katibu
huyo amebainisha kuwa mabondia walioshinda mapambano yao kwa knockout (KO) katika
michuano hiyo ni Maneno Athuman na Musa Haruna.
Bageleza
amesema bondia mmoja amepoteza pambano lake na mwingine anasubiri ratiba ya pambano lake.
Hata
hivyo ameulaumu uongozi wa serikali ya mkoa wa Tabora kwa kushindwa kuisaidia
kifedha timu hiyo ambayo imekwenda kuwakilisha mkoa wa Tabora.
Hata hivyo Bageleza
amewataka wapenda michezo na wadau kuisaidia timu hiyo ili iweze kufanya vizuri
katika hatua nyingine ya michuano hiyo.
Akizungumza kwa njia ya simu mmoja wa mabondia hao Bakari Athumani amesema kuwa walilazimika kuuza baadhi ya vitu vyao ili kupata fedha za kujikimu wakiwa safarini na kwenye mashindano hayo.
1 comment:
Hivi mko wapi apa Tabora tujiunge na wengine
Post a Comment