Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Monday, February 22, 2016

MANCHESTER UNITED YAFANIKIWA KUTINGA HATUA YA ROBO FAINALI YA FA CUP, RATIBA YA UEFA CHAMPS LEAGUE



JUAN MATA AKISHANGILIA BAO LA PILI
Manchester United imefanikiwa kusonga mbele hatua ya robo fainali ya michuano ya kombe la FA (EMIRATES FA CUP) baada ya kuifunga timu ya Shrewsbury Town kwa mabao 3 kwa 0 kwenye mechi iliyochezwa Jumatatu.
 
Wachezaji vinara waliyoifungia Manchester United  ni Chris Smalling aliyefunga bao la kwanza katika dakika ya 37, Juan Mata alitikisa nyavu za wapinzani na kuandika bao la pili kunako dakika ya 47 na goli la tatu na la ushindi lilipachikwa na Jesse Lingard katika dakika ya 61 ya mchezo.

Robo fainali ya kombe la FA itatimua vumbi tarehe 12 ya mwezi ujao ambapo Manchester United ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford itaikaribisha West Ham United.

Katika hatua hiyo ya robo fainali (au nane bora) Everton wakiwa nyumbani Goodison Park wataikaribisha Chelsea,Reading watakuwa kwenye uwanja wao wa Madejski wakivaana na Crystal Palace na timu ya Wartford inasubiri mshindi wa mechi ya marudiano kati ya Arsenal na Hull City itakayochezwa Jumanne ya tarehe 8 mwezi ujao baada ya kutoka suluhu ya kutokufungana siku ya Jumamosi.

RATIBA YA LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA 

JUMANNE  23 Februari 2016

Juventus
v
FC Bayern Munchen
Juventus Stadium
22:45

Arsenal
v
Barcelona
Emirates Stadium
22:45


JUMATANO 24 Februari 2016

Dynamo Kyiv
v
Manchester City
Kiev Olympic Stadium
22:45

PSV
v
Atletico de Madrid
Philips Stadion
22:45

No comments: