![]() |
LUIS SUAREZ NA LIONEL MESSI WAPIGA HAT-TRICK |
Mechi ya kwanza ya Nusu fainali ya Kombe la Mfalme
Copa Del Rey nchini Hispania imezikutanisha timu za Barcelona na Valencia.
Katika mechi hiyo yameshuhudiwa magoli 7 yakifungwa ambapo Lionel Messi amefunga magoli 3 na Luis Suarez magoli 4.
Magoli hayo 7 yameufanya ubao wa matangazo
kusomeka Barcelona 7 na Valencia 0 hadi filimbi ya mwisho inapulizwa.
Katika mechi ya marudiano itakayochezwa terehe 10
mwezi huu inaifanya Valencia kufunga magoli zaidi ya 8 ili iweze kusonga mbele
kwenye hatua ya fainali.
Leo nusu fainali ya pili itazikutanisha timu za
Sevilla na Celta Vigo mechi itakayochezwa majira ya saa 4:30 usiku kwa saa za
afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment