Na
Ramadhan Faraji, Tabora.
Ligi
daraja la tatu ngazi ya mkoa wa Tabora imeanza kutimua vumbi katika uwanja wa Ally Hassan Mwinyi Jumatano
jioni watoto wa mjini, Tabora FC
walikutana uso kwa uso na wabishi wa mjini, Saba saba FC.
Mechi
hiyo ilikuwa na ushindani wa hali ya juu na kuvuta hisia za mashabiki wengi wa Soka mjini
Tabora ilimalizika kwa watoto wa mjini, Tabora FC kuwatambia wabishi wa mjini
kwa kuwalaza kwa bao 3 kwa 1.
Iliwachukua
dakika 4 za mchezo Saba Saba FC kumlazimisha mwamuzi wa kati wa mechi hiyo
Rajabu Hussein kutoa ishara ya mpira uwekwe kati baada ya Mashaka Juma kupiga
shuti kali nje ya penati box na kuiandikia timu yake bao la kwanza lilidumu kwa
dakika 36.
Tabora
FC walipata bao la kusawazisha kupitia kwa mchezaji wao Ajubi baada ya
kuunganisha kwa kichwa mpira wa krosi na kumuacha golikipa wa Saba Saba FC
Kilanga Mavumbi akigaa gaa asijue la kufanya.
Hadi
timu hizo zinakwenda mapumziko zilikuwa zimefungana bao 1 kwa 1, kupindi cha
pili kilianza kwa kasi huku washambuliaji wa timu zote wakijituma kupata magoli
ya ushindi kwa timu zao.

Dakika
90 zilimalizika na ubao wa matokeo kusomeka Tabora FC 3 na Saba Saba FC 1.
Kikosi
cha Tabora FC kinanolewa na kocha Andrew Zoma na Saba Saba FC inafundishwa na
kocha Mohamed Mdoma.
No comments:
Post a Comment