Na Deogratius Yagomba, Tabora
Msanii wa kizazi kipya mkoani Tabora Haruna J.
Mabokela maarufu kama "Mabokela" amesaini mkataba wa miaka
mitatu na meneja wake mpya Abubakar Ally maarufu kwa jina la “Beka T the Boss.”
Akizungumza na Tabora Watch ilipomtembelea ofisini
kwake Mabokela amesema anaimani muziki
wake sasa utafika mbali kwa kupata mkataba na meneja anayejua kazi ya muziki.
Msanii huyo amebainisha kuwa hatua hiyo itamsogeza
karibu zaidi na mashabiki wake ambao wamekuwa wakimkubali kwa kazi zake na
namna anavyomiliki jukwaa kwenye “Live Show.”
Mabokela licha ya kuvipongeza vyombo vya habari
kumtangaza na kucheza kazi zake amevilaumu baadhi ya vyombo hivyo kutotoa
ushirikiano wa kutosha kwa wasanii wanaoibukia kwa visingizio mbalimbali
ikiwemo ubora wa kazi.
Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya ameweka wazi kuwa lengo lake kubwa ni kuhakikisha muziki wake
unatambulika katika mipaka ya Tanzania na kisha kuvuka nje mipaka hiyo kwa kuwa
uwezo wa kufanya hivyo anao.
Ameomba wadau kuendelea kumuunga mkono kwa kuwa amekwisha
andaa nyimbo mpya zikiwa kwenye hatua ya mwisho za matayarisho ya video zake na
zitakapokamilika zitasambazwa kwenye vituo mbalimbali vya redio na television.
Katika hatua nyingine Mabokela amefurahishwa kuono
mtangazaji wa BBC Salim Kikeke kupost wimbo wake unaojulikana kama 'SIZE YAKO
kwenye mitandao ya kijamii ili wadau wamsikilize.
Amesema hatua hiyo imempa imani kubwa kuwa kazi
anayo ifanya watu wanamuelewa.
Mabokela ametamba na vibao vingi kama Azizi,Maisha
Hadohado,Niambie , Size yako na vingine
vingi.
No comments:
Post a Comment