Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Tuesday, February 16, 2016

TFF YAIPONGEZA AFRICAN LYON FC KWA KUPANDA LIGI KUU MSIMU UJAO



AFRICAN LYON

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeipongeza timu ya African Lyon FC ya jijini Dar es salaam kwa kufanikiwa kupanda ligi kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao, baada ya kuwa vinara wa Kundi A katika ligi hiyo iliyomalizika Jumapili.

African Lyon imeungana na timu ya Ruvu Shooting FC ya Mlandizi mkoa wa Pwani iliyokua timu ya kwanza kupanda ligi kuu wiki iliyopita kutoka kundi B.

TFF inaitakia kila la kheri Africa Lyon FC katika maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara.

Africa Lyon kwenye ligi hiyo ya VPL itaungana na timu nyingine 15 ambapo kila klabu kitacheza jumla ya michezo 30 nyumbani na ugenini kwa msimu wa 2016/2017.

No comments: