Featured Post

KITUMBO:MAWASILIANO MADHUBUTI YA KIUTAWALA NI SIRI YA MAFANIKIO

Na Paul Christian, Tabora. Mawasiliano mazuri ya kiutawala baina ya wenyeviti na watendaji wa mitaa na wananchi ni jambo muhimu kat...

Tuesday, February 23, 2016

MZALENDO "LAWYER J. BOKILO" ATAKA MAGUFULI KUONGEZEWA ULINZI, KAZI YA KUTUMBUA "MAJIPU" INAMTENGENEZEA MAADUI

J. F. KENNEDY
Kupitia Group la WhatsApp linalojulikana “Tabora Ndio Kwetu” mmoja wa washiriki wa Group hilo "Lawyer J. Bokilo" mnamo tarehe 22 Februari, 2016 alionyesha wasiwasi wake kiusalama kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi anayoifanya ya kutumbua “MAJIPU” huku akionekana kutembea wakati mwingine katika maeneo yenye Usalama Mdogo. 

Kazi hiyo ya kutumbua “MAJIPU” inamtengenezea maadui wenye nguvu ya fedha na ushawishi, ni vyema tahadhari za kimsingi za kiusalama zikachukuliwa.

Bokilo alitoa mfano wa Rais wa 35 wa Marekani J.F.Kennedy aliyeuawa mwaka 1963.

"Wazo hilo la Kizalendo limenifanya nipitie historia ya Dunia kubaini namna baadhi ya WAKUU WA NCHI walivyouawa kwa hila wakiwa madarakani wakiwahudumia wananchi wao."

BAADHI YA WAKUU WA NCHI WALIOUAWA WAKIWA MADARAKANI KATI YA MWAKA 1865 NA MWAKA 2011:

#
JINA LA MKUU WA NCHI
SIKU YA KUUAWA AU SHAMBULIO
AINA YA MAUAJI AU MUUAJI
1.
14 Aprili, 1865
Rais wa 16 wa Marekani alipigwa risasi kichwani na John Wilkes Booth alipokuwa akiangalia mchezo wa kuigiza na alifariki siku iliyofuata tarehe15 Aprili,1865. Muuaji John Wilkes Booth alifanyikiwa kutoroka lakini baadae alipigwa risasi na kufa.
2.
 2 Julai, 1881.
Rais wa 20 wa Marekani alipigwa risasi na Charles J. Guiteau, lakini Rais huyo aliweza kuishi hadi tarehe 19 Septemba ambapo alifariki kwa sumu kwenye mzunguko wa damu yake. Charles J. Guiteau alishitakiwa kwa mauaji na baadae kuhukumiwa kunyongwa  tarehe 30 Juni, 1882.
3.
6 Septemba,
1901
Rais wa 25 wa Marekani alipigwa risasi mara mbili na Leon Czolgosz wakati  akitembelea maonyesho ya Pan-American yaliandaliwa Buffalo, New York.Rais huyo alikufa tarehe 14 Septemba, 1901.Muuaji alishitakiwa na kuhukumiwa kupigwa shot ya umeme hadi kufa tarehe  29 Oktoba, 1901.
4.
22  Novemba,
1963
Rais wa 35 wa Marekani aliuawa kwa kupigwa risasi na Lee Harvey Oswald,wakati akiwa kwenye msafara wake Dallas, Texas. Baadae Jack Ruby alimpiga risasi na kumuua Oswald kabla hajafikishwa mahakamani.
5.
Hara Takashi
4 Novemba, 1921
Waziri mkuu wa 10 wa Japan alichomwa kisu na Nakaoka Kon'ichi katika Station ya Tōkyō. Muuaji aliachiwa huru miaka 13 baadae.
6.
Inukai Tsuyoshi
15 Mei,1932
Waziri mkuu wa Japan. Alipigwa risasi na askari 11 wa jeshi la nchi hiyo akiwa kwenye makazi ya waziri mkuu katika jiji la Tokyo.
7.
Paul Doumer
7 Mei,1932
Rais wa Ufaransa aliuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye ufunguzi wa maonyesho ya Vitabu yaliyofanyika kwenye Hôteli ya Salomon de Rothschild jijini Paris na wakati huo akizungumza na mwandishi wa vitabu Claude Farrère ambapo Paul Gorguloff alifyatua risasi kadhaa na mbili zilimpata Rais huyo chini ya fuvu la kichwa na nyingine kwenye kwapa la kulia alianguka chini na baadae kufariki akiwa hospitalini jijini Paris.
8.
Crown Prince Louis Rwagasore
13 Oktoba, 1961
Waziri mkuu wa pili wa taifa la Burundi.Aliuawa akiwa anapata chakula cha usiku katika Hoteli club du lac Tanganyika katika jiji la Bujumbura, Burundi.
9.
Sylvanus Epiphanio Olympio
13 Januari, 1963
Rais wa Togo. Usiku wa manani Rais huyo aliamshwa na kundi la askari wa jeshi la nchi hiyo na kabla ya mapambazuko mwili wake uligunduliwa na balozi wa Marekani nchini humo Leon B. Poullada ukiwa umbali wa futi tatu nje ya mlango wa ubalozi wa Marekani.
10.
Pierre Ngendandumwe
15 Januari, 1965
Waziri mkuu wa Burundi aliuawa na mkimbizi wa kitusi kutoka Rwanda baada ya kuchaguliwa kuhudumu muhula wa pili wa wadhifa huo tarehe 7 Januari, 1965.
11.
Alhaji Sir Abubakar Tafawa Balewa
15 Januari, 1966
Waziri mkuu pekee wa Nigeria huru alipinduliwa na kuuawa na wanajeshi,mwili wake ulipatikana kando kando ya barabara jijini Lagos siku sita baada ya tukio hilo.
12.
François Tombalbaye
13 Aprili,1975
Rais wa Chad. Aliuawa na wanajeshi wa nchi hiyo.
13.
Park Chung-hee
26 Oktoba, 1979
Rais wa Korea ya Kusini aliiongoza nchi hiyo tangu mwaka 1961. Aliuawa kwa kupigwa risasi na mkurugenzi wa shirika la kijasusi la Korea KCIA Kim Jae-gyu.
14.
Muhammad Anwar El Sadat
6 Oktoba, 1981
Rais wa Misri aliuawa na askari wakati wa gwaride lilifanyika Cairo katika kusheherekea nchi hiyo kuvuka upande wa pili wa mfereji wa Suez.
15.
Indira Priyadarshini Gandhi
31 Oktoba, 1984
Waziri mkuu pekee mwanamke wa India. Aliuawa na walinzi wake wawili Satwant Singh na Beant Singh, kwa kumpiga risasi akiwa kwenye bustani ya makazi ya waziri mkuu yaliyopo barabara ya 1 Safdarjung , New Delhi.
16.
Sven Olof Joachim Palme
28 Februari, 1986
Waziri mkuu wa 26 wa Sweden. Aliuawa akiwa anatoka kuangalia sinema akiwa na mke wake Lisbet Palme ambapo walivamiwa na muuaji na kuwafyatulia risasi, wakati huo waziri mkuu huyo hakuwa na ulinzi.
17.
Thomas Isidore Noël Sankara
15 Oktoba, 1987
Rais wa Burkina Faso (1983-1987). Aliuawa kwa kupigwa risasi na kundi la askari walilokuwa na silaha katika mapinduzi yaliyoongozwa na rafiki yake wa zamani Blaise Compaoré.
18.
21 Oktoba, 1993
Rais wa kwanza wa Burundi aliyechaguliwa kidemokrasia na wa kwanza kutoka kabila wa Wahutu aliapishwa tarehe 10 Julai, 1993. Alipinduliwa na kuuawa na jeshi la Burundi.
19.
Juvénal Habyarimana
6 Aprili, 1994
Rais wa Rwanda aliingia madarakani 1973.Aliuawa baada ya ndege aliyokuwa akisafiria kutunguliwa karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kigali katika ndege hiyo pia alikuwemo Rais wa Burundi Cyprien Ntaryamira.
20.
Cyprien Ntaryamira
6 Aprili, 1994
Rais wa Burundi aliyeingia madarakani tarehe 5 Februari, 1994. Aliuawa kwenye ndege  pamoja na Rais wa Rwanda Juvénal Habyarimana.
21.
Agathe Uwilingiyimana
7 Aprili 1994
Waziri mkuu wa kwanza na akiwa mwanamke wa kwanza wa Rwanda. Alishika madaraka hayo tangu tarehe 18 Julai,1993 hadi kifo chake.Aliuawa katika mauaji ya kimbari.
22.
Yitzhak Rabin
4 Novemba, 1995
Waziri mkuu wa Tano wa Israel. Alihudumu misimu miwili katika wadhifa huo  1974-1977 na kisha 1992 hadi kifo chake.Aliuawa kwa kupigwa risasi tatu na Yigal Amir.Rabin alikuwa akihudhuria mkusanyiko wa Umma katika uwanja wa wafalme wa Israel (sasa hivi unajulikana kama Rabin Square) kwa lengo la kuunga mkono Makubaliano ya Oslo.
23.
Laurent-Désiré Kabila
16 Januari, 2001
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo tangu tarehe 17 Mei, 1997 baada ya kumfurusha Mobutu Sese Seko.Aliuawa na mmoja wa walinzi wake.
24.
João Bernardo "Nino" Vieira
2 Machi, 2009
Rais wa Guinea-Bissau .Alihudumu nafasi hiyo kwa mihula mitatu 1980-1984,1984-1999 na 2005-2009.Aliuawa na askari wa jeshi la nchi hiyo.
25.
Muammar Muhammad Abu Minyar al-Gaddafi
20 Oktoba, 2011
Rais wa Libya tangu mwaka 1969 hadi 2011.Aliuawa na wanamgambo wa Misratan baada ya kushindwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

No comments: