![]() |
MJI WA TABORA |
Na
Allan Ntana, Tabora
MKOA
wa Tabora umefanikiwa kuandikisha jumla ya watoto 53,581 wa kuanza elimu ya
awali katika mwaka wa masomo 2016 .
Hayo
yamebainishwa hivi karibuni na afisa elimu mkoa wa Tabora Juma Mhina katika
kikao cha wadau wa elimu kilichoketi hivi karibuni mjini hapa kikishirikisha
maofisa kutoka halmashauri zote 7 za mkoa huo.
Amesema
idadi hiyo ni ya watoto imeandikishwa katika halmashauri zote za mkoa huo
ambapo idadi halisi ya watoto waliotarajiwa kuandikishwa ni 74,773 wavulana
wakiwa 37,581 na wasichana 37,192.
Katika
makisio hayo afisa elimu huo amesema wavulana walioandikishwa ni 21,664 sawa na
asilimia 57.6 na wasichana ni 21,917 sawa na asilimia 58.9 ambapo jumla ya
watoto wote walioandikishwa katika wilaya zote ni 53,581 sawa na asilimia 71.6.
Amefafanua
kuwa halmashauri ya Manispaa ya Tabora imefanikiwa kuvuka lengo la makisio yake
ambapo watoto waliotarajiwa kuandikishwa ni 4,881 lakini walioandikishwa ni 5,099
sawa na asilimia 104.5.
Mbali
na Manispaa, ametaja takwimu za makisio ya kila halmashauri na idadi halisi ya
watoto walioandikishwa ikiwa kwenye mabano kama ifuatavyo Igunga 17,844
(11,675), Nzega 16,643 (7,586), Urambo 8,433 (4,517), Sikonge 6,446 (2,227),
Uyui 8,206 (4,801), Kaliua 9,944 (5,758) na Nzega Mji 2,376 (1,916).
Akizungumzia
zoezi la uandikishwaji watoto wa kuanza darasa la kwanza Mhina amesema Mkoa huo
umefanikiwa kuandikisha jumla ya watoto 64,642 sawa na asilimia 70.6 wakati
matarajio ilikuwa kuandikisha watoto 91,506.
Aidha
Mhina ameipongeza halmashauri ya Manispaa Tabora kwa kufanikiwa kuvuka lengo la
uandikishaji ambapo iliandikisha watoto 7,644 sawa na asilimia 110 wakati
matarajio yalikuwa kuandikisha watoto 6,924.
Ametaja
takwimu za watoto walioandikishwa darasa la kwanza kwa kila halmashauri idadi
iliyotarajiwa ikiwa kwenye mabano kama ifuatavyo Sikonge 2,569 (5,288), Kaliua
10,522 (16,042), Uyui 10,217 (16,571), Urambo 7,301 (8,844), Manispaa 7,644
(6,924), Igunga 11,675 (17,844), Nzega 12,678 (16,898) na Nzega Mji 2,036
(2,111).
No comments:
Post a Comment