Na Magreth
Kinabo – Nzega
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee Dk. Hamisi
Kigwangalla amesema wataendelea kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli kutumbua majibu yanayokwamisha kupatikana kwa huduma
bora za afya ,bila kuogopa wala kumwonea mtu kwa ajili ya maslahi ya
taifa.
Amesema watafanya hivyo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ili
kuhakikisha kila mtu anatimiza wajibu ipasavyo.
Dk.Kigwangalla
ametoa kauli hiyo Alhamis wakati wa maadhimisho ya 24 ya ibada maalum ya
kuwaombea wagonjwa Duniani ambayo Kitaifa yamefanyika katika jimbo Kuu la
Tabora na baadae kwenye Hospitali ya Ndala, iliyopo Kata ya Ndala, Wilaya
ya Nzega, Mkoani Tabora.
“ Tutaendelea kutumbua majibu bila ya kmwonea mtu kwa kuwa
tunafanya hivyo kwa kuangalia sheria, kanuni na taratibu. Haiwezekani mtu
akaiba dawa ambazo zinawasaidia wananchi masikini, halafu sisi tukamwaangalia
tu,” amesema Dkt.Kigwangalla.
Amesema majipu hayo yatatumbuliwa kwa watendaji ambao
watakaozembea, wasio waadili na wasiowajibika katika sekta hiyo ya afya.
Ameongeza kwamba Serikali ya Awamu ya Tano itakuwa inafanya kazi
kwa kuwafuata wananchi hususan wanyonge (masikini) mahali walipo ili
kuhakikisha baada ya miaka kumi ijayo Tanzania itakuwa na maendeleo ya kiwango
cha juu.
Naibu Waziri huyo amewaomba viongozi wa dini kuendelea kuwaombea
kwa kuwa kazi ya kutumbua majibu si rahisi.
Dkt. Kigwangalla meuomba uongozi wa hospitali hiyo kuboresha mfumo
wa ukusanyaji mapato kwa kutumia vifaa vya elekroniki kwa sababu umeonyesha
matokeo chanya katika hospitali nyingine.
Akizungumzia kuhusu suala la upungufu wa bajeti,Dkt. Kigwangalla
amesema ni vyema viongozi hao wadini, asasi za kijamii na taasisi zisizoza
kiserikali zinazotoa huduma za afya kutafuta vyanzo mbadala vya kuongeza fedha
za kuboresha huduma hizo, kwa kuwa si sekta hiyo pekee yenye changamoto hiyo.
Pia vipaumbele vya shughuli mbalimbali za kuwaletea maendeleo
wananchi viko vingi, wakati rasilimali fedha haitoshelezi.
Amewataka uongozi wa hospitali hiyo na nyinginezo za mashirika ya
hiari kuwasilisha taarifa za (data cleaning) UTUMISHI ikiwa ni pamoja na
kuorodhesha watumishi wanaotakiwa kuondolewa kwenye malipo ya mshahara
ili waweze kupatiwa kibali cha kuajiri kwani bila kufanya hivyo kibali
hakitaweza kutolewa.
Dkt. Kigwangalla ameongeza kwamba hivi sasa wizara yake iko katika
mchakato wa kuhakikisha Watanzania wote wanapata huduma za matibabu za
kwa kutumia mifuko ya bima ya afya. Hivyo Februari 20,mwaka huu
Maadhimisho
hayo ni ya kila mwaka ya siku 11 Februari, Wakristo wote wanafanya sala maalum
ya kuwaombea wagonjwa wanaosumbuka na maradhi na kuwaombea wapone haraka
huku wakiyapokea mateso hayo na kuyaunganisha na mateso ya kristo na kanisa
lake hii ni pamoja na kuwaombea ndugu wa wagonjwa katika kuwasaidia wagonjwa
wao wakati wa kuwauguza.
Maadhjimisho
hayo yanaenda sambamba pamoja na kuwahudumia na kutoa misaada mabalimbali.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ludocivk Mwananzila amewataka Watanzania kuwa na
tabia ya kuwatembelea wagonjwa na wafungwa ili waweze kupata faraja.
Kihistoria,
Hospitali hiyo ya Ndala, ilianza miaka ya 1930 kama Zahanati ndogo chini ya
Masista Wamissionary wa Afrika (Missionary of Our Lady of Afrika-White Sisters)
katika jimbo kuu hilo la Tabora
Mwaka 1963
ilikuja kuwa Hospitali kamili huku ikianza na vitanda 115 na wauguzi 15 na daktari
mmoja, hata hivyo hadi sasa ina jumla ya vitanda 152, wafanyakazi 125 huku wakiweza
kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje wapatao 38,917 na wagonjwa wakulazwa 8,428.
Hospitali hiyo na baadae
ikapandishwa ngazi ya Hospitali huku ikiwa na vitanda 152 huku ikiwa na
madaktari mbalimbali.
Wakitoa
shukrani zao ni pamoja na serikali ya Tanzania kupitia wizara ya afya kwa
kuweza kushirikiana bega kwa bega ikiwemo kutoa ruzuku kwa baadhi ya watumishi,
posho za watumishi, vitanda vulivyohainishwa, madawa, mafunzo ya watumishi, na
mambo mbalimbali
No comments:
Post a Comment